ZIC YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Bi Saada Mkuya (Kulia) akiwaongoza maofisa waandamizi pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kukabidhi msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya sh mil 30 kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja iliyopo visiwani humo ikiwa ni sehemu maadhimisho ya 53 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Bw Marijani Msafiri , Mkurugenzi wa Bima ya Kawaida wa ZIC, Bw Jape Khamis (Katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya ZIC Bw Ramadhani Mwalimu Khamis.


Tukio hilo lilipambwa na maandamano ya amani yaliyoongozwa na Waziri Saada Mkuya (katikati) kutoka makao makuu ya Shirika hilo hadi hospitali ya Mnazi Mmoja na kisha maandamano hayo yalirejea tena kwenye ofisi ya makao makuu ya shirika hilo ambapo yalihitimishwa kwa furaha na pongezi miongoni mwa washiriki wote.


Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye viunga vya hospitali hiyo, Waziri Saada Mkuya (pichani) pamoja na kulipongeza shirika hilo linalomilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), alisema msaada huo ni uthibitisho tosha kuwa shirika hilo linajiendesha kwa faida huku likitimiza vema malengo ya kuanzishwa kwake.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya (ZIC) Bw Ramadhani Mwalimu Khamis (pichani) alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wateja wa shirika hilo katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.


Awali akizungumza kwenye hafla hiyo fupi Mkurugenzi wa Bima ya Kawaida wa ZIC, Bw Jape Khamis (pichani) aliemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo alisema kupitia maadhimisho hayo shirika hilo limekuwa karibu zaidi na wadau wake muhimu wakiwemo wateja ambapo pamoja na msaada huo shirika hilo pia limetoa msaada wa zawadi mbalimbali za papo kwa papo kwa wateja.


Akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Bw Marijani Msafiri (Pichani) mbali na kulipongeza shirika hilo kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake, alisema msaada huo utaongeza tija zaidi katika utoaji wa huduma za kiafya hospitalini hapo kutokana na uhaba wa vifaa hivyo huku pia baadhi ya vifaa vikiwa vinakabiliwa na changamoto ya uchakavu.


Tukio hilo lilipambwa na maandamano ya amani yaliyoongozwa na Waziri Saada Mkuya kutoka makao makuu ya Shirika hilo hadi hospitali ya Mnazi Mmoja na kisha maandamano hayo yalirejea tena kwenye ofisi ya makao makuu ya shirika hilo ambapo yalihitimishwa kwa furaha na pongezi miongoni mwa washiriki wote.

.............................................

Na Mwandishi Wetu-Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Bi Saada Mkuya hii leo amewaongoza maofisa waandamizi pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kukabidhi msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya sh mil 30 katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja iliyopo visiwani humo ikiwa ni sehemu maadhimisho ya 53 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo.

Vifaa hivyo ni pamoja na taa inayosaidia upasuaji, kifaa cha uangalizi wa wagonjwa wa dharura pamoja na mashine za kupima shinikizo la damu.

Tukio hilo lilipambwa na maandamano ya amani yaliyoongozwa na Waziri huyo kutoka makao makuu ya Shirika hilo hadi hospitali ya Mnazi Mmoja na kisha maandamano hayo yalirejea tena kwenye ofisi ya makao makuu ya shirika hilo ambapo yalihitimishwa kwa furaha na pongezi miongoni mwa washiriki wote.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo iliyofanyika kwenye viunga vya hospitali hiyo, Bi Saada pamoja na kulipongeza shirika hilo linalomilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), alisema msaada huo ni uthibitisho tosha kuwa shirika hilo linajiendesha kwa faida huku likitimiza vema malengo ya kuanzishwa kwake.

“Pamoja na kutumia maadhimisho haya kujiweka karibu zaidi na wateja wenu, nimefurahishwa zaidi kuona kwamba mmeamua kutenga sehemu ya faida yenu ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wanaopigania afya zao hospitalini. Hii imekuwa ni moja ya sababu iliyonisukuma kuungana nanyi hii leo…hongereni sana ZIC kwa kuwa mnegeweza tu kujipongeza wenyewe ila mkaona ni vema mlichokipata mkirejeshe kwa jamii kupitia jambo hili muhimu,’’ alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Bw Ramadhani Mwalimu Khamis alisema hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na wadau mbalimbali wakiwemo wateja wa shirika hilo katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

“Shirika la Bima Zanzibar tunaamini kupitia wananchi hawa, ndipo biashara yetu inapofanikiwa hivyo basi tuna wajibu wa kuchangia maendeleo ya nchi hii kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya afya. Changamoto za sekta ya afya kwetu ni jambo la kipaumbele, kwa kuwa afya ndio msingi wa uchumi na uzalishaji mali na ni kichocheo kikuu cha maendeleo ya wananchi.’’ Alisema.

Awali akizungumza kwenye hafla hiyo fupi Mkurugenzi wa Bima ya Kawaida wa ZIC, Bw Jape Khamis aliemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo alisema kupitia maadhimisho hayo shirika hilo limekuwa karibu zaidi na wadau wake muhimu wakiwemo wateja ambapo pamoja na msaada huo shirika hilo pia limetoa msaada wa zawadi mbalimbali za papo kwa papo kwa wateja.

“Katika tukio linguine kubwa ambalo ndio litahitimisha kilele cha maadhimisho haya tumeandaa hafla maalum tikilenga kukutana na wateja wetu katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo visiwani hapa kwa ajili ya kujipongeza kwa pamoja, kupata mrejesho kutoka kwa wateja kuhusu huduma zetu, kujadili fursa za biashara pamoja na kuzindua Program maalum ya mtandaoni kwa ajili ya huduma za shirika yaani Online Application.’’ Alisema

Akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Bw Marijani Msafiri mbali na kulipongezas shirika hilo kwa kutimiza miaka 53 tangu kuanzishwa kwake, alisema msaada huo utaongeza tija zaidi katika utoaji wa huduma za kiafya hospitalini hapo kutokana na uhaba wa vifaa hivyo huku pia baadhi ya vifaa vikiwa vinakabiliwa na changamoto ya uchakavu.

“Miongoni mwa vifaa hivi ni pamoja na taa zinazosaidia upasuaji ni upasuaji ambazo kiukweli zinapatikana kwa shida hivyo kupitia msaada huu tutaokoa maisha ya wananchi wengi. Zaidi pia tunashukuru kwa msaada wa vifaa vya uangalizi wa wagonjwa wa dharura hususani wale changamoto ya COVID 19 kwa kuwa mashine hii ni muhimu katika kuonesha kiasi cha hewa ya oxygen kilichopo kwenye mapafu ya mgonjwa’’ alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post