Watu watano wamefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya kupata ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Wish (Mchomoko) ambayo imetokea Jana majira ya saa 10 jioni eneo la Ruguru Wilayani Itilima Mkoani Simiyu.
Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Blasius Chatanda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema chanzo cha tukio hilo ni mwendokasi.
Hata hivyo kamanda Chatanda amesema katika ajali hiyo watu watatu walifariki papo hapo huku wengine wawili wakifariki wakati wakipatiwa matibabu na majeruhi wengine wanaendelea na matibabu.
Social Plugin