DKT. MAGEMBE AWAJULIA HALI WANAFUNZI WA KING DAVID WALIOPATA AJALI..IDADI YA VIFO YAONGEZEKA

Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Dkt. Grace Magembe (wa tatu kulia) akiwajulia hali wanafunzi wa Shule ya Msingi King David ambao wamepata ajali mapema leo tarehe 26 Julai 2022.
Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , Dkt. Grace Magembe ametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula kuwajulia hali wanafunzi wa Shule ya Msingi King David ambao wamepata ajali mapema leo tarehe 26 Julai 2022.

Wanafunzi hao wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo na hali zao zinaendelea kuimarika.

Aidha Dkt. Magembe anatoa salamu za pole kwa wazazi ndugu na Jamaa ambao wameondokewa na watoto wao.

Mganga mkuu wa mkoa wa Mtwara Dkt. Mohamed Nyembea amethibitisha kuongezeka kwa vifo vya mwanafunzi wawili wa shule ya msingi ya King David, ambao walikuwa miongoni mwa majeruhi watano waliokuwa katika hali mbaya wanaopartiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa huo, Ligula.


Vifo vya wanafunzi hao vinafanya idadi ya vifo kufikia watu 13, ambao ni wanafunzi 11 na wengine wawili ambao ni dereva na
msaidizi wake.

Majeruhi watano wamehamishiwa katika hospitali ya Ndanda kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi baada ya hali kuwa mbaya.

Habari zaidi kutoka Mtwara zinaeleza kuwa miili ya wanafunzi hao imeagwa alasiri ya leo katika hospitali ya rufaa ya Ligula.

Watu hao wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi mkoani Mtwara baada ya basi dogo la shule kutumbukia kwenye korongo katika eneo la mteremko la Mjimwema kata ya Magengeni, Mikindani mkoani Mtwara wakati wakielekea shuleni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post