JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATOKEO YA MAOMBI YA AJIRA MPYA ZA KADA ZA AFYA ZILIZO CHINI YA USIMAMIZI WA
MOJA KWA MOJA WA WIZARA YA AFYA
Dodoma, Alhamisi Juni 30, 2022.
Mnamo Mwezi Aprili, 2022 Wizara ya Afya, ilipata kibali cha kuajiri jumla ya nafasi 1,650 za Wataalamu wa kada mbalimbali ambao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya. Huu ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kibali cha nafasi hizo za ajira 1,650 kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI kilitoa fursa kwa wataalamu wa kada mbalimbali katika vituo vilivyo chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Wizara ya Afya. Kati ya nafasi hizo, nafasi 29 ambazo hazihusiani na afya moja kwa moja zitatangazwa na Sekretariati ya Ajira na hivyo kubaki nafasi 1,621 chini ya Wizara ya Afya pekee.
Kada za afya ambazo zitanufaika na nafasi hizi ni; Madaktari, Wafamasia, Wateknolojia wa Dawa, Wateknolojia wa Maabara, Wateknolojia wa Mionzi, Wateknolojia wa Macho, Maafisa Uuguzi, Watoa Tiba kwa Vitendo, Wazoeza Viungo kwa Vitendo, Maafisa Afya Mazingira pamoja na Wasaidizi wa Afya.
Baada ya kupokea kibali hicho, Wizara ilitangaza nafasi 1,621 za kada ya afya kupitia tovuti ya Wizara ya ajira.moh.go.tz kuanzia tarehe 16-29 Aprili, 2022. Hata hiyo, kutokana na umuhimu wa zoezi hili Wizara iliongeza muda hadi tarehe 03 Mei, 2022 ambapo ilikuwa ndiyo siku ya kufungwa kwa mfumo. Mpaka tangazo lilipofungwa jumla
Ukurasa wa 1 kati ya 7
2
ya waombaji 19,464 ndiyo walikamilisha taratibu za uombaji kwenye mfumo na waombaji 8,404 hawakukamilisha taratibu za uombaji.Kati ya waombaji 19,464 waliofanyiwa uchambuzi, waombaji 7,897 walikidhi vigezo vya awali kama ilivyoorodheshwa hapa chini:
i. Kuzingatia Miundo ya Utumishi kwa kada za Afya (Alama 3).
ii. Waombaji waliohitimu masomo yao kuanzia Mwaka 2020 kurudi nyuma isipokuwa Madaktari Bingwa, Wahandisi Vifaa Tiba, Fundi Sanifu Vifaa Tiba, Watekinolojia na Walemavu (Alama 2.5).
iii. Waombaji wenye ulemavu (Alama 1.5)
iv. Watumishi walioajiriwa kwa mkataba na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wanaofanya kazi kwa makubaliano ya kuajiriwa kupitia vibali vya ajira vinapotolewa na ikiwa wamekidhi sifa. (Alama 1.5).
v. Waombaji wenye umri mkubwa (kati ya miaka 35 hadi 44) na waliokidhi vigezo. (Alama 1).
Hatua hiyo ilifatiwa na uchambuzi wa kina na jumla ya waombaji 1,605 walichaguliwa, wanaume 921(57%) na wanawake 684(43%) kwa kutumia vigezo vya ziada vifuatavyo: i. Waombaji waliopata alama za juu kupitia vigezo vilivyoainishwa awali wakati wa zoezi la uchambuzi.
ii. Waombaji walioonesha nia ya kwenda kufanya kazi kwenye maeneo ya vipaumbele yalioainishwa kwenye tangazo la kazi.
iii. Waombaji wenye nia ya kwenda kufundisha katika Vyuo vya Afya. iv. Waombaji wanaojitolea katika Hospitali za Mikoa ya pembezoni.
Nafasi 16 za Madaktari bingwa, hazikupata waombaji hivyo, nafasi hizo zitajazwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za ajira katika Utumishi wa Umma.
Aidha, watumishi hawa waliochaguliwa wamepangiwa vituo vya kazi kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
i. Uanzishwaji wa Hospitali mpya za Kanda Mtwara na Chato.
ii. Ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa.
Ukurasa wa 2 kati ya 7
3
iii. Upanuzi wa majengo mapya katika Hospitali za zamani (Sekou Toure (Mwanza), Mawenzi (Kilimanjaro), Maweni (Kigoma), Mbeya Mkoa na Kanda, Kibongoto, Mirembe (Dodoma).
iv. Mahitaji ya watumishi wanaohitajika katika Hospitali mbalimbali za Kanda, Maalumu na Mikoa ukilinganisha na wagonjwa wanaopata huduma. Hii ni pamoja na upungufu wa watumishi katika vyuo vya Afya.
v. Kuongezeka kwa vifaa tiba vya kisasa ambavyo vinahitaji wataalamu wa kuvitumia vifaa hivyo.
Mgawanyo wa watumishi kwa kila hospitali ni kama unavyoonekana katika jedwali hapa chini;
Ukurasa wa 3 kati ya 7
4
CHUO CHA MAAFISA TABIBU MUHIMBILI DAR ES
25
SALAAM 3
Ukurasa wa 4 kati ya 7
5
66 HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SHINYANGA 38
Ukurasa wa 5 kati ya 7
107
6
MWANZA SCHOOL OF HEALTH AND ALLIED
SCIENCE 3
Mgawanyo wa watumishi watakaopelekwa katika Hospitali za Kanda, Maalum, Mikoa, Vyuo, Mipakani na Vituo vya Damu Salama vya Kanda ni kama ifutavyo;
Ukurasa wa 6 kati ya 7
7
Sababu zilizochangia baadhi ya waombaji wengine kukosa ajira
i. Baadhi ya waombaji wa ajira kutojaza kabisa au kutojaza kwa ukamilifu namba za usajili zilizotolewa na Mabaraza yao hivyo kusababisha kushindwa kutambuliwa.
ii. Baadhi ya waombaji kufanya makosa ya kutumia namba za usajili za wanataaluma wengine wanaotambulika na Baraza au kutumia namba za mtahiniwa zilizotumika wakati wa mitihani ya Baraza au chuo.
iii. Waombaji kuomba nafasi za ajira ambazo hawana sifa nazo. Mfano mwombaji mwenye sifa ya Stashahada kuomba nafasi ya Shahada (Skills mismatch). iv. Wapo ambao hawakukidhi vigezo vya miuundo.
Majina ya waombaji wote waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Afya www.moh.go.tz.
Prof. Abel N. Makubi
KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA
Ukurasa wa 7 kati ya 7