Iwapo umedurusu mitandao ya kijamii, huenda umekutana na video ya mzee mmoja kwenye simu yake akimtaka aliyempigia kukata simu kwa kutumia neno "Kata simu kata simu tupo site we don't like disturbance of the head you understand."
Tayari wanamtandao wengi wanatumia msemo huo kama meme, video, na pia katika majukwaa ya kisiasa ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa manifesto ya kiongozi wa chama cha Roots George Wajackoyah. Aliyeanzisha msemo huo ni msanii mcheshi, Umar Iahbedi Issa almaarufu Mzee Mjegeje mwenye kutoka nchini Tanzania.
Akizungumza katika mahojiano ya awali, Mzee Megeje alibainisha kuwa anavutiwa na sanaa na anataka kuunda maudhui ambayo yanawavutia hadhira.
Mjegeje aliyezaliwa na kukulia huko Bagamoyo, Tanzania, alijieleza kuwa ni mfanyabiashara ambaye alitafuta riziki kutokana na ujasiriamali. Kabla ya kujitosa kwenye sanaa, mchekeshaji huyo mwenye utata alikuwa anamiliki hoteli kubwa nchini Tanzania ambayo ni biashara yenye faida ambayo alikuwa ameweka akiba yake ili kuanzisha.
Hoteli hiyo yenye makao yake makuu katikati ya jiji la Tanga, ilionekana kuwa eneo la kimkakati huku wateja mbalimbali wakimiminika kwa ajili ya kupata chakula. Hata hivyo, alidai kuwa wafanyikazi wake walihusudu mafanikio ya biashara yake na walipanga mpango wa kuangusha biashara yake. Wakati huo, alikuwa akijishughulisha na mipango ya harusi na mpenzi wake, na hivyo kuacha biashara chini ya uangalizi wa wafanyikazi. Alidai kuwa wafanyakazi hao waliharibu biashara yake.
“Nilikuwa na mali nyingi lakini kwa kusalitiwa na marafiki na wafanyakazi, waliniacha na madeni makubwa yaliyoniacha katika hali mbaya ya kifedha.” "Kwa muda wa miezi mitatu, sikuondoka nyumbani kutokana na wakusanyaji wa madeni walikuwa wakinitafuta," alisimulia. Akifunga duka, Megeje alibainisha kuwa alijitosa katika muziki na ubunifu wa maudhui kwa kutumia ujuzi wake wa kuchekesha.
Mchekeshaji huyo alifichua kuwa alitengana na mkewe, lakini akabainisha kuwa bado wana uhusiano mzuri na pamoja wamejaliwa mtoto mmoja.
Aliwashauri vijana kufanya kazi kwa bidii na kujipatia kipato kutokana na jasho lao na pia alisisitiza umuhimu wa kitengo cha familia katika jamii.
Social Plugin