Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BETWAY YAADHIMISHA MWAKA MMOJA TANZANIA, YAZINDUA JACKPOT YA KIHISTORIA


Jimmy Masaoe, Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania (mwenye suti nyeusi) akiwaongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kukata keki kama ishara ya kuadhimisha mwaka mmoja wa Betway nchini Tanzania. Hafla ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa Betway Tanzania ilifanyika jioni ya Jumatano Julai 27 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubashiri Tanzania, James Mbalwe akizungumza na washiriki wa hafla ya kuadhimisha mwaka mmoja wa Betway Tanzania (hawapo pichani). Mbalwe alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jioni ya Jumatano Julai 27 jijini Dar es Salaam.

***

Betway inayomilikiwa na Super Group, ambayo ni kampuni maarufu ya kimataifa ya ubashiri na bahati nasibu katika michezo mtandaoni imetimiza mwaka mmoja tangu izinduliwe rasmi nchini Tanzania. Katika hafla fupi ya kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo nchini Tanzania iliyofanyika Jumatano Julai 27, 2022 jijini Dar es Salaam, Betway ilizindua huduma na bidhaa mpya ikiwemo Betway Jackpot na jukwaa jipya la kubashiri kidigitali.  

Tangu ilipoingia Tanzania, Betway imetekeleza mambo kadhaa makubwa ikiwemo ukarabati wa viwanja vya michezo, ufunguzi wa kituo cha kisasa cha kushuhudia michezo, pamoja na kuunda ushirikiano na mamlaka za michezo na wadau ili kukuza maendeleo ya michezo nchini. Sambamba na hayo, kampuni ya Betway imechangia katika uboreshaji wa sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha kwa kuanzisha huduma bora za kuwezesha ubashiri kupitia majukwaa ya kidigitali. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyowakutanisha zaidi ya wadau 50 wa sekta ya ubashiri na michezo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliipongeza kampuni ya Betway kwa jitihada za kukuza maendeleo ya michezo nchini Tanzania na kuitaka kampuni hiyo kuendelea kuwa mfano mzuri kwa makampuni mengine. Vilevile Mbalwe alitoa rai kwa Betway na makampuni mengine ya ubashiri na michezo ya kubahatisha kuisaidia Bodi hiyo katika utekelezaji kanuni na sera zinazolenga kukuza uwajibikaji katika sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha. 

“Sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha kwa sasa inakua kwa kasi, katika miongo miwili iliyopita ya kuanzishwa kwa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kumekuwa na upanuzi wa shughuli za ubashiri na michezo ya kubahatisha. Ukuaji huu umechangia ongezeko kubwa la ukusanyaji wa mapato ambapo sekta ya michezo ya kubahatisha ilipata ukuaji wa asilimia 20.69 katika ukusanyaji wa ushuru wa michezo ya kubahatisha kutoka TZS 78.8 bilioni mwaka 2017/18 hadi TZS 95.1 bilioni mwaka 2018/19. Haya ni mafanikio makubwa ambayo hayawezi kupuuzwa. Mbali na hayo, sekta hii imeibua fursa za ajira kwa Watanzania, imevutia uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje, na kuchangia katika maendeleo ya teknolojia kupitia uhamishaji wa teknolojia unaofanywa na makampuni haya yanapokuja kuwekeza Tanzania", alisema Mbalwe.

“Tunawapongeza Betway kwa sababu katika kipindi cha mwaka mmoja wamefanikiwa kuweka historia nzuri katika sekta ya ubashiri na michezo ya kubahatisha hasa kwa kushika kibendera na kuendeleza dhana ya uwajibikaji katika ubashiri, kuleta teknolojia za kisasa za kidigitali, kuanzisha mazingira ya kisasa ya kushuhudia michezo, na muhimu zaidi kuchangia uboreshaji wa miundombinu ya michezo. Haya ni mambo ya kupongeza, tunatumai kampuni nyingine za ubashiri na michezo ya kubahatisha zitajifunza kupitia Betway.” aliongeza Mbalwe.

Kwa upande mwingine, Betway ilitumia fursa hiyo kutambulisha bidhaa zake na huduma zake mpya ikiwa ni pamoja na Betway Jackpot, jukwaa jipya la kubashiri kidigitali, mabalozi wapya, na kampeni mbili ambazo ni kampeni ya Chomoka na Odds na nyongeza ya 700% kwa wateja wa kampuni hiyo. Akizungumzia mwelekeo mpya uliotangazwa kampuni hiyo, Calvin Mhina ambaye ni Meneja Masoko wa Betway Tanzania alisema.

“Kulingana na utafiti wetu na uzoefu tuliokusanya katika kipindi cha mwaka mmoja, tumekuja na bidhaa za kusisimua zaidi ambazo zitawafaa wateja wetu. Kwa kuanza, tumezindua jukwaa jipya la kubashiri kwa urahisi zaidi kidigitali ili kuwarahisishia huduma wateja wetu. Pia tumezindua jackpot kubwa zaidi nchini yenye zawadi kubwa zaidi ya TZS 5,000,000,000, ili kuwapa wateja wetu machaguo zaidi na uwezekano mkubwa zaidi wa kuboresha maisha yao kupitia ubashiri na michezo ya kubahatisha. Hatua nyingine kubwa ambayo tumefanya leo ni kuzindua odds mpya na kuongeza kiwango cha ushindi kwa 700%. Tunatumai haya yataendekea kuongeza chachu ya maendeleo ya sekta ya kamari nchini Tanzania.” alisema Mhina.

Kupitia hafla hiyo iliyopambwa na huduma mbalimbali za kimichezo, Betway pia ilitambulisha waraghibishi wawili wapya kwa lengo kukuza uhamasishaji wa elimu ya kubashiri kistaarabu pamoja na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo. Waraghibishi wapya waliotambulishwa na Betway ni Priva Shayo (Privaldihno) na George Ambangile - wote wawili ni watangazaji na wachambuzi wa michezo.

Wadau waliohudhuria hafla hiyo walifurahia huduma mbalimbali za michezo na baadhi yao kujishindia zawadi za hadi TZS 100,000 kupitia mashindano mbalimbali ya michezo yaliyokuwa sehemu ya hafla hiyo. 

Kuhusu Betway Group
Betway ni sehemu ya Super Group: kampuni ya kimataifa ya kidijitali ambayo hutoa huduma ya daraja la kwanza ya kubashiri na bahati nasibu katika michezo..

Super Group (SGHC) Limited ni kampuni inayoongoza duniani katika biashara ya kubashiri michezo mtandaoni na bahati na nasibu: Betway, chapa kubwa ya kubashiri michezo mtandaoni na Kasino. Imeorodheshwa kwenye New York Stock Exchange (NYSE ticker: SGHC), kampunii imepewa leseni katika maeneo zaidi ya 20, ikiwa na nafasi za juu katika masoko makubwa kote Ulaya, Amerika na Afrika. 

Mafanikio ya kikundi katika kubashiri michezo na bahati nasibu za mtandaoni yanachagizwa na teknolojia nzuri ili kuiwezesha kuingia haraka na kwa ufanisi katika masoko mapya. Teknolojia yetu husaidia katika upembuzi yakinifu wa taarifa za masoko huiwezesha kutoa huduma za kipekee kwa wateja. Kwa maelezo zaidi, tembelea www.sghc.com 

Betway Group ni mtoa huduma anayeongoza kwa huduma nzuri na ya kibunifu katika kubashiri michezo, kasino na esports. Ilianzishwa mwaka wa 2006, na inafanya kazi katika idadi ya masoko ya mtandaoni yaliyodhibitiwa. Betway inajivunia kutoa huduma na bora kwa wateja wake inayochagizwa na mazingira rafiki, salama, haki na uwajibikaji.

 Betway ni mwanachama wa taasisi kadhaa katika tasnia, ikiwemo International Betting Integrity Association (IBIA), iGaming European Network (iGEN), Independent Betting Adjudication Service (IBAS), Sports Wagering Integrity Monitoring Association (SWIMA) na Betting na Gaming Council (BGC), na inatambuliwa kwa ISO 27001 kupitia wakala wa vipimo na viwango anayeaminika wa kimataifa eCOGRA. 

Betway Tanzania, inasimamiwa na Media Bay Limited imepewa Leseni na kusimamiwa na Wizara ya Fedha na Mipango, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ya Tanzania. 

Kwa taarifa zaidi kuhusu Betway, tembelea: www.betway.co.tz

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com