Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BANK OF AFRICA YAWAPATIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAFANYABIASHARA MKOANI MWANZA


Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Adam Mihayo, akifungua warsha ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara wateja wa benki hiyo iliyofanyika jijini Mwanza.
***

BANK OF AFRICA-TANZANIA imeendesha warsha ya uwezeshaji wajasiriamali iliyolenga wafanya biashara wadogo na wakati (SME) mkoa wa Mwanza. Tukio hili liliwakutanisha pamoja wateja mbalimbali wa benki hiyo ambao ni Wafanyabiashara Wadogo na wa Kati (SME) na kuwapatia ujuzi na maarifa muhimu kwa ukuaji mzuri na thabiti ya biashara zao.

Washiriki kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mwanza, walijengewa uwezo kuhusu masuala ya kifedha ikiwemo mbinu za utunzaji fedha, namna ya kukuza mtaji na kushirikiana ili kukua pamoja kibiashara.

Akifungua warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa BANK OF AFRICA, Bw. Adam Mihayo, aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabiashara nchini kuchangamkia huduma za kifedha zitolewazo na Benki hiyo ili kuongeza tija.

"Sisi BANK OF AFRICA, katika mpango mkakati wa miaka mitatu ni kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi. Sekta ya wafanyabiashara wadogo na wakati ni sekta muhimu na nyeti katika uchumi wetu inachangia asilimia 30% katika pato la taifa. Ukiangalia takwimu katika biashara 10, 9 zitatokea kwa wafanya biashara wadogo na wakati. 

Nawakaribisha Bank of Africa kwa kuwa ndiyo benki yenye mtazamo chanya unaolenga kuwasaidia wajasiriamali wadogo na wakati, hii ni katika huduma zetu madhubuti kwenye sekta hii kuanzia ufunguaji wa akaunti ya benki, mikopo, ufumbuzi wa kibiashara na ushauri katika kukuza na kustawisha biashara za wajasiriamali. Karibuni tuwahudumie” alisema, Bw Adam Mihayo.


Bw. Adam Mihayo, pia alisema kwa kipindi cha mwaka jana Benki ilitoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 32 kwa wajasiriamali wadogo na wakati, ukilinganisha na mwaka huu mpaka juni mwaka huu tayari imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 23 huu ni mwenendo mzuri na tunatumaini kwamba mpaka mwisho wa mwaka tutakua tumetoa kiasi kikubwa zaidi.

“Katika mpango mkakati wa miaka mitatu pia tumepanga kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 132 kwa sekta hii nyeti na tunaamini katika kufanya hivyo tunachangia ukuaji wa uchumu wetu. 

Dhumuni kubwa la warsha hii ni kuwawezesha wafanyabiashara wa jijini Mwanza ambao ni wateja wetu katika maeneo mbali mbali, utafiti unaonyesha kwamba biashara nyingi hazifanikiwi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati ni kutotunza kumbukumbu vizuri, wanapata changamoto ya mahesabu yao, kunachangamoto pia ya dhamana. Mada za warsha hii zitawawezesha kuendesha biashara zao kwa ufanisi zaidi.

Tunaamini kwamba sisi kama BANK OF AFRICA, tunaendelea vizuri kibiashara. Ukiangalia mahesabu yetu tumeweza kukuza mizania yetu (balance sheet) mpaka kufikia shilingi bilioni 711, ukuaji ambao hatujawahi kufikia, faida yetu pia imekua kwa asilimia 37 ukilinganisha juni mwaka jana faida ya shilingi bilioni 3.4 na Juni mwaka huu ya shilingi bilioni 4.7. Tunaendelea kuboresha huduma zetu ili kufikia mahitaji ya wateja wetu” alisemaBw. Mihayo.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria warsha hiyo, wameipongeza BANK OF AFRICA, kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa BOA, Bi. Ninael Mndeme, amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Baadhi wa Wajasiriamali waliohudhuria warsha ya kuwajengea uwezo kibiashara iliyoandaliwa na BOA wakifuatilia mada mbalimbali.
Afisa Mtendaji Mkuu wa River Oil Gabriel Kenene (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa Waandamizi wa benki ya BOA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Adam Mihayo (wa pili kutoka kulia) wakati walipomtembelea ofisini kwake.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Khalii(kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Bank Of Africa (BOA), Adam Mihayo alipomtembelea ofisini kwake jijini Mwanza.
Mkurugenzi Mtendaji Wa BOA,Adam Mihayo akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com