Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA KIPEPEO PAD YAGAWA TAULO ZA KIKE SHULE YA WASICHANA JANGWANI

Kampuni ya Kipepeo Pad inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike imetoa na kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam.

Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika shuleni hapo Julai 27,2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani ambaye ametumia fursa hiyo kuwasihi wanafunzi hao wa kike kusoma kwa bidii na kuepuka vishawishi ili watimize ndoto zao huku akiishuru Kampuni ya APS kwa kutoa msaada huo wa taulo za kike.


Mkurugenzi wa kampuni ya Kipepeo Pad Janeth Dutu aliyeambatana na mwakilishi wa Taasisi ya Girls Chapter amesema uhitaji wa taulo za kike kwa mabinti bado ni mkubwa katika shule mbalimbali huku akiwasihi kuzingatia matumizi sahihi ya taulo za kike na kujitunza ili watimize ndoto zao
Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Charangwa Selemani akizungumza wakati Kampuni ya Kipepeo Pad ikitoa na kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kipepeo Pad, Janeth Dutu akizungumza na wanafunzi wa shule Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kipepeo Pad Janeth Dutu akizungumza na wanafunzi wa shule Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kipepeo Pad, Janeth Dutu akifurahia jambo baada ya kugawa taulo za kike 1700 kwa wanafunzi wote wa shule ya sekondari ya wasichana Jangwani Girls Secondary School Jijini Dar es salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com