Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DAKTARI MATATANI TUHUMA ZA KUMBAKA MAMA MJAMZITO AKIMFANYIA UPASUAJI


Mwanamke mjamzito
Daktari Quentella Bezerra aliyetuhumiwa kuhusika na ubakaji wa mjamzito alikamatwa hospitali humo
13 Julai 2022


Onyo: Baadhi ya maudhui huenda yakawaathiri baadhi ya wasomaji


Daktari wa ganzi alikamatwa mapema Jumatatu asubuhi baada ya kushtakiwa kwa kumbaka mgonjwa aliyelazwa wakati wa upasuaji katika Hospitali ya Wanawake ya Heloneida Studart huko Rio de Janeiro.


Kwa mujibu wa Polisi, mwanamume huyo alinaswa na ujumbe wa usaidizi wa Wanawake wa jiji hilo, baada ya uhalifu huo kurekodiwa kwenye video.


Maafisa wa polisi walikimbilia katika kituo hicho baada ya maafisa wa kitengo cha afya ambao walikuwa wakihofia utendaji wa daktari huyo wa ganzi na kumpiga picha wakati wa upasuaji.


Daktari huyo alitambuliwa na mamlaka kuwa Giovanni Quintella Bezerra.


Kulingana na kitengo cha Habari kilichofanikiwa kupata kanda hiyo ya video wakati wa tukio la uhalifu , mtu huyo aliingiza uume wake katika kinywa cha mwanamke huyo wakati alipokuwa katika ganzi.


Polisi walisema kwamba Quintella Bezerra alituhumiwa kwa tukio la ubakaji dhidi ya mtu ambaye alikuwa hawezi kujitetea. Anakabiliwa na kifungo jela cha kati ya miaka 8 hadi 15.



Wakili wa Bezerra amesema kwamba atazungumzia tukio hilo baada ya kuchunguza taarifa na ushahidi uliopo. Hatahivyo wakili huyo baadaye aliambia BBCNews Brazil kwamba alijiondoa katika kesi hiyo, na BBC imeshindwa kumpata wakili mpya wa mtuhumiwa.

Kipi kilichotokea?


Kulingana na maafisa wa polisi wa jiji la Rio de Jeneiro , Quintella Bezerra anatuhumiwa kumbaka mwathiriwa wakati alipokuwa akijifungua.


Katika kanda ya video iliotolewa , mwathiriwa alikuwa amepoteza fahamu katika kitanda cha upasuaji . Shuka inayotumiwa wakati wa upasuaji hutumika kuficha sehemu ya juu ya mwanamke na ile ya chini.


Katika picha hizo , upande wa kushoto wa shuka hilo, kundi la madaktari wa upasuaji wanaonekana wakifanya upasuaji huo.


Lakini upande wake wa kulia, umbali wa chini ya mita moja kutoka kwa wenzake, mtu aliyetambulika katika kanda hiyo ya video kama daktari huyo wa ganzi , anaonekana amesimama karibu na uso wa mwanamke huyo.


Kulingana na video hiyo, daktari huyo alifungua zipu ya suruali yake ndefu akatoa uume wake na kuuingiza katika kinywa cha mwanamke huyo. Taaarifa hiyo ilisema kwamba kitendo hicho kilichukua takriban dakika 10 . Mwishowe mtu huyo alionekana akimsafisha mwathriwa na karatasi ili kufuta Ushahidi wa uhalifu huo.

Je alirekodiwa vipi?


Kanda ya video ilirekodiwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa polisi na wauguzi wa kitengo hicho.


Wauguzi hao walificha simu ndani ya kitengo hicho cha upasuaji baada ya kuwa na wasiwasi kuhusu kiwango cha ganzi alichotumia daktari huyo wakati wa upasuaji na utendaji wake wakati alipokuwa karibu na mgonjwa huyo.


Kulingana na G1 , maafisa wa hospitali hiyo walibadilisha chumba cha kujifungua ili kurekodi kitendo hicho katika kanda ya video.


Siku ya Jumapili, daktari huyo alihusika katika upasuaji mwengine katika vyumba ambavyo ingekuwa vigumu kurekodi video za siri.

Je alikamatwa vipi?


Kundi la maafisa wa polisi waliomkamata afisa huyo wa matibabu lilitumwa kuthibitisha kwamba daktari huyo wa ganzi alimlaza kwa dawa mjamzito huyo wakati wa upasuaji na kumnyanyasa.


‘’Mara moja maafisa hao waliingia katika hospitali hiyo na kubaini wauguzi waliingiza simu na kurekodi kitendo cha daktari huyo wakati wa upasuaji kwasababu hawakumuamini’’, ilisema Taarifa iliotolewa na maafisa wa polisi.

Katika video ya wakati wa kukamatwa kwake ,daktari huyo alishangaa kupokea hati ya kukamatwa ambayo afisa wa polisi Barbara Lomba alimpa wakati akielezea kwamba amerekodiwa akimdhulumu mgonjwa.


Chupa zilizokuwa na dawa hiyo ya ganzi zilichukuliwa huku maafisa wa hospitali hiyo wakilazimika kutoa Taarifa.


Pia daktari huyo alichunguzwa iwapo alihusika na uhalifu mwengine.

Je daktari huyo ni nani?


Kulingana na Waziri wa afya wa jiji kuu la Rio de Jeneiro , Giovanni Quintella Bezerra ni daktari wa ganzi na alifanya kazi miezi sita iliopita katika hospitali ya wanawake ya Heloneida Studart na hospitali nynegine mbili katika eneo hilo.

"Daktari huyo si mtumishi wa serikali," sekretarieti ilisema katika taarifa. Ana cheo cha mtaalamu wa anesthesiolojia na amesajiliwa kama mtaalamu wa kawaida.


Uongozi wa Hospitali ya Wanawake ulianzisha uchunguzi wa ndani ili kuchukua hatua za kiutawala na kuarifu Baraza la Mkoa la Tiba la jimbo la Rio de Janeiro.


Baraza hilo lilitoa maelezo ya kuthibitisha kupokea malalamishi hayo na likafungua mara moja utaratibu wa tahadhari ya kusimamishwa kazi mara moja kwa daktari huyo, kutokana na uzito wa kesi hiyo.


"Mchakato wa maadili ya kitaaluma pia unaanzishwa, ambao hukumu yake ni uhamisho wa huduma zake za kitaaluma," shirika hilo lilisema.


Katika barua iliyotumwa kwa G1, watetezi wa daktari huyo walisema kwamba bado hajapata taarifa na ushahidi uliotolewa wakati wa mchakato wa kukamatwa kwake.


"Upande wa utetezi pia unaarifu kwamba, baada ya kupata nyenzo zote, utatoa taarifa dhidi ya shtaka lililotolewa dhidi ya daktari huyo."


Wakili huyo baadaye aliambia BBC News Brasil siku ya Jumatatu kwamba hakuwa akimwakilisha tena Bezerra katika kesi hiyo.

CHANZO - BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com