Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALIYEHIFADHI MWILI WA MAMA YAKE NDANI NA KUENDELEA KUSALI AFUFUKE AKAMATWA





Polisi katika kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 45 kwa kuhifadhi mwili wa mamaake na kusali kuwa afufuke.

James Muchira na mkewe walikamatwa katika kijiji cha Mutithi usiku wa Jumatatu, Julai 4, 2022 baada ya jamaa zao wakiongozwa na nduguye Evans Mwaniki kumwomba naibu chifu wa eneo hilo kuingilia kati.

Kwa mujibu wa ripoti, mshukiwa alikataa kumruhusu yeyote katika makaazi yake ambayo pia huhudumu kama kanisa kwa jina "God's mountain of Believers."

“Maafisa wangu walishtuka kupata mwili uliooza,” kamanda wa polisi wa kaunti ndogo Mwea Magharibi Wilson Koskei.

Mshukiwa anaripotiwa kumtoa mamaake hospitalini ambako alikuwa akipokea matibabu ili amwombee katika kanisa lake la nyumbani.

“Siamini katika kanisa lake la familia,” Mwaniki alisema. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com