Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WARUNDI WAUAWA TUKIO LA UJAMBAZI KIGOMA


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Mendrad Sindano (kushoto) akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (kulia) kuhusu tukio la ujambazji wa kutumia bunduki lililotokea wilayani Kakonko mkoani Kigoma ambapo watu wawili raia wa Burundi waliuawa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Mendrad Sindano akionesha bunduki iliyokamatwa katika tukio la ujambazi lililotokea wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma ambapo watu wawili wanaodhaniwa kuwa raia wa Burundi waliuawa kuhusika na tukio hilo.
Bunduki aina ya AKA 47 iliyokamatwa kwenye tukio la uporaji kijiji cha Bukirillo wilaya ya Kakonko ambapo majambazi wawili wanaosadikiwa kuwa raia wa Burundi waliuawa wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo. (Picha na Fadhili Abdallah)


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imewaua kwa risasi watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wakituhumiwa kuhusika na tukio la uporaji kwa kutumia bunduki kwenye soko la kijiji cha Bukirilo wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma lililopo mpakani mwa Tanzania na Burundi.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Menrad Sindano akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini Kigoma amesema kuwa tukio hilo lililotokea juzi majira ya saa mbili usiku kijijini hapo ambapo majambazi waliouawa wanadaiwa kuwa ni raia wa Burundi.

Sindano alisema kuwa katika tukio hilo majambazi hao wakiwa watatu wakitumia budnuki aina ya AKA 47 walipora vitu mbalimbali ikiwemo vitenge, simu na pesa taslimu katika maduka matatu likiwemo dula la dawa, vitenge na kibanda cha M-pesa.

“Baada ya tukio hilo wananchi waliripoti tukio hilo kituo cha polisi Gwanumpu wakiomba msaada baada ya kuwazingira majambazi hao wakiwarushia mawe ndipo askari polisi na jeshi kutoka kikosi cha mpakani cha Bukirilo walifika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi ambapo majambazi wawili walijeruhiwa vibaya na mmoja alifanikiwa kukimbia,”Alisema Kamanda Sindano.

Alisema kuwa baada ya majibizano ya risasi na majambazi hayo kujeruhiwa walifariki njiani wakipelekwa hospitali ya wilaya Kakonko ambapo msako unaendelea kumtafuta jambazi mmoja aliyekimbia.

Katika tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma alisema kuwa walifanikiwa kukamata bunduki moja aina ya AKA 47 ikiwa na magazine mbili na risasi 15 sambamba na maganda matatu ya risasi, simu tisa walizokuwa wamepora na fedha taslimu shilingi 82,000/

Kamanda Sindano alisema kuwa katik upekuzi huo marehemu hao walikutwa na vitambulisho viwili kwenye nguo zao na kutaja majina kwenye vitambulisho hivyo kuwa ni Harelimana Ananias (30) na Nimpangalitse Jean (36) wakazi wa mkoa Ruyigi nchini Burundi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com