Haji Manara Msemaji wa Yanga
Saleh Ally ‘Jembe’
MCHAMBUZI wa soka nchini Saleh Ally ‘Jembe’ amesema Haji Manara anapaswa kujiweka mbali na marafiki wanafiki ambao wanamjaza upepo (Kumdanganya) kwamba hana makosa kutokana na hukumu aliyoipata ya kufungiwa miaka miwili kutojihusisha na soka pamoja na faini ya shilingi milioni 20.
Akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Global TV, Jembe amenukuliwa akisema:
“Mimi natakuwa tofauti na rafiki zake wengine wote, natakakuwa tofauti na rafiki zake especially rafiki zake wanafiki rafiki ambao badala ya kumuambia kitu sahihi cha kufanya wanazidi kumpoteza zaidi kwa kufuata masuala ya kishabiki kwasababu tunaona kweli Haji amekosea na kama amekosea imefikia hatua Haji amehukumiwa hatuwezi kuwa watu wazuri kama tutakuwa tunafurahia kuhukumiwa kwa Haji badala yake tunatakiwa kuwa watu ambao tunatakiwa kumueleza ukweli.”
Aidha Jembe amemtahadharisha Manara kuhusu kutaka kushindana na Mamlaka ya soka nchini kwani kwa kufanya hivyo hawezi kufanikiwa kwa lolote na hakutakuwa na manufaa au afya kwa maendeleo ya soka nchini.
Jembe amemshauri Manara kujitathmini na kuzingatia maelekezo ya Mamlaka ya soka kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kutengeneza mazingira ya yeye kuja kusamehewa baadaye kwani tayari kuna ushahidi wa watu wengi ambao walishawahi kufungiwa na baada ya kuonesha mwenendo mzuri wakafunguliwa vifungo vyao na mmoja wapo ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela.
Social Plugin