Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MUME ADAIWA KUMUUA MKEWE KWA KUMKATA KATA MAPANGA



Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Toba Nguvila ameliagiza jeshi la Polisi Wilaya ya Muleba kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kumkamata mwanaume anayedaiwa kumuua mke wake kwa kumkatakata mapanga.


Mauaji hayo yametokea usiku wa kuamkia Jumamosi Julai 09, 2022 katika Kijiji Kasheno Kata ya Magata Karutanga Wilayani Muleba Mkoani Kagera ambapo Bi.Zaidia Swaibu (35) anadaiwa kuuawa kwa kukatwa na mapanga na Mume wake Swaibu Mswadiko (48) ambaye mpaka sasa hajulikani alipo.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kufika katika eneo la tukio Dc Nguvila ameagiza Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Kimila wa eneo hilo kukutana na kujadili mustakabali wa usalama wa wananchi katika Kata ili kutokomeza vitendo vya mauaji.

"Huyu aliyefanya kitendo hiki ni lazima sheria za nchi zichukuliwe dhidi yake, kuua ni kosa la jinai hatuwezi kumuacha ni lazima atafutwe popote alipo hivyo naagiza Jeshi la Polisi kumtafuta mtuhumiwa na akipatikana utaratibu wa sheria na kanuni kwa mujibu wa Katiba yetu uchukue mkondo wake" amesema Mhe. Nguvila.
Aidha, ameagiza wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa atakayemuona mtuhumiwa huyo kutoa taarifa ili akamatwe na hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.

"Mimi Mkuu wa Wilaya na Kamati yangu ya Usalama kitendo hiki kimetufedheesha sana, sihitaji kuona tukio jingine kama hili likifanyika tena na aliyefanya hiki kitendo atakapooonekana popote pale toeni taarifa haraka ili akamatwe.

Chanzo - Lango la Habari

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com