Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limemkamata Seleman Malima maarufu “Jiwe” mkazi wa Keko Mwanga kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Husna Majaliwa mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa maeneo ya Goba kwa Awadhi kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali Tumboni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo huku akisema tukio hilo limetokea Juni 12, 2022 maeneo ya Goba kinondoni.
Amesema mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alitoroka na juhudi za kumtafuta zilianza na kufanikiwa kumkamata Julai 18, 2022 katika maeneo ya Mbande Jijini Dodoma.
Kamanda Muliro amesema uchunguzi wa awali umethibitisha kulikuwa na mgogoro wa kifamilia baina ya wawili hao na mtuhumiwa alifika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kumsalimia mzazi mwenzake pamoja na mtoto.
Wakati wakiwa kwenye maongezi ndipo mtuhumiwa Seleman alimshambulia mke wake kwa kisu na kumsababishia kifo.
Social Plugin