Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kwa ajili ya kuukimbiza Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi kwenye miradi ya maendeleo ambayo itapitiwa na Mwenge huo.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
MWENGE wa Uhuru umeanza kukimbizwa mkoani Shinyanga, katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, kwa kuzindua na kuweka Mawe ya Msingi kwenye Miradi ya Maendeleo, na hakuna hata mradi mmoja ambao umekataliwa.
Mwenge huo umepokelewa leo Julai 26, 2022 ukitokea Mkoani Geita, na umepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, katika viwanja vya michezo shule ya Msingi Mwakitolyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule, na kisha kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Akizungumza mara baada ya kuupokea Mwenge huo wa Uhuru,Mjema amesema mkoani Shinyanga utakimbizwa Kilomita 838 na utapitia Jumla ya Miradi ya Maendeleo 38 yenye thamani ya Sh.bilioni 43.1.
Aidha, akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa huo Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko , amesema, Mwenge utakimbizwa Wilayani Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga Kilomita 202, na utazindua Miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya Sh.bilioni 34.2.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akikagua Miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, amesema ameridhishwa na Miradi hiyo.
"Miradi ambayo imeonekana ina mapungufu madogo madogo irekebishwe haraka, na ile ambayo haijakamilika imaliziwe ili ianze kutoa huduma kwa wananchi, Miradi yote ni mizuri nimeridhishwa nayo," amesema Geraruma.
Katika hatua nyingine Kiongozi huo Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Geraruma, amewataka wananchi siku ya kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi Agosti 23 mwaka huu, wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa.
Miradi ya Maendeleo ambayo imepitiwa na Mwenge huo wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, ni ujenzi wa Mradi wa Majisafi na salama kutoka Ziwa Victoria katika kijiji cha Mwakitolyo namba tano.
Miradi mingine ni ujenzi wa Jengo la dharura na nyumba Nne za Watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga, kituo cha Mafuta cha mtu binafsi Kishushu pamoja na uzinduzi Klabu ya Mazingira Shule ya Msingi Iselamagazi.
Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu (2022) inasema "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki kuhesabiwa kwa Maendeleo ya Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, (Wa pili kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Rosemary Senyamule, Kulia ni kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma (katikati) akizungumza mara baada ya kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kulia) ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Edward Ngelela.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma, akizungumza na Wanafunzi katika Shule ya Msingi Iselamagazi wilayani Shinyanga mara baada ya kumaliza kuzindua Klabu ya Mazingira shuleni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye uzinduzi na kuweka Mawe ya Msingi kwenye Miradi ya Maendeleo ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, (katikati) akiwa katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo inapitiwa na Mwenge wa Uhuru, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, na (wapili kulia) ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, (kulia) Mbunge wa Viti maalumu Christina Mzava.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi kwenye Tangi la Mradi wa Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria katika kijiji cha Mwakitolyo namba Tano, (kulia) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma,akiweka Jiwe la Msingi kwenye Tangi la Mradi wa Majisafi na Salama kutoka Ziwa Victoria katika kijiji cha Mwakitolyo namba Tano, pembeni yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy.
Muonekano wa Tangi la Maji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa kituo cha Mafuta cha Mtu Binafsi kilichopo Iselamagazi, kulia ni Mkurugenzi wa kituo hicho Bundala Kishushu
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika ujenzi wa nyumba Nne za watumishi katika Hospitali ya wilaya ya Shinyanga na Jengo la wagonjwa wa dharura.
Muonekano wa Jengo wa wagonjwa wa dharurua katika Hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Muonekano wa nyumba za watumishi katika Hospitali ya wilaya ya Shinyanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akipanda Mti katika Shule ya Msingi Iselamagazi alipofika kuzindua Klabu ya Mazingira shuleni hapo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, akikabidhi Cheti kwa mwakilishi wa Klabu ya Mazingira Shule ya Msingi Iselamagazi mara baada ya kumaliza kuzindua Klabu hiyo.
Muonekano wa Miti ambayo imepandwa na Klabu ya Mazingira katika shule ya Msingi Iselamagazi.
Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo ukiendelea.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, (kulia) akiendelea kukagua miradi ya maendeleo kabla ya kuizundua na kuweka mawe ya msingi, (kushoto) ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.
Ukaguzi wa miradi ya maendeleo ukiendelea.
Ukaguzi wa miradi ya maendeleo ukiendelea.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 Sahili Nyanzabara Geraruma, (wa tatu kushoto) akifurahi jambo wakati akipitia nyaraka kwenye ukaguzi wa miradi, (kushoto) ni Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava, akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (kushoto) ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga ukitokea Geita.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nice Munissy, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava, akiwa ameushika Mwenge wa Uhuru.
Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akiushika Mwenge wa Uhuru.
Social Plugin