Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye, atoa wito kwa wananchi kuendelea huduma za Shirika la Posta kwani kwa sasa Shirika limeboresha huduma zake kuwa za kisasa kulingana na mahitaji ya wananchi.
Hayo ameyasema leo Tarehe 06 Julai, 2022 wakati alipohudhuria Siku maalum ya Shirika la Posta katika viwanja vya Maonesho ya 46 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam
Aidha, Mhe. Waziri ametumia nafasi hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa juhudi inayoendelea kuzifanya katika kutoa huduma bora na stahiki kulingana na mahitaji ya wananchi hususani katika kipindi hiki cha maendelea ya TEHAMA
Sambamba na hilo, Mhe. Nape amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali viwanjani hapo ikiwemo Banda la Shirika la Posta Tanzania na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika viwanja hivyo
Naye, Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo ameelezea huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo viwanjani hapo ikiwemo huduma za EMS, Duka Mtandao, Posta Kiganjani, Huduma za kubadilisha fedha za kigeni na Uwakala ikiwemo ukataji wa tiketi za ndege ya ATCL
Pia, Postamasta Mkuu ametumia nafasi hiyo kuendelea kuwakaribisha wananchi katika banda la Posta lililopo viwanjani hapo ili kuendelea kufurahia huduma za kisasa
Hafla hiyo ya Siku maalum ya Posta imehudhuriwa Viongozi waandamizi na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania pamoja na wasanii mbalimbali wa maigizo (Bongo Movie) ikiwemo Swebe, Snura, Tausi Mdegela, Dr Kumbuka, Asha Boko, na wengine mbalimbali
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania.
06 Julai, 2022.
Social Plugin