Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi, linamtafuta mkazi wa mtaa wa Jangwani, Halmashauri ya Manispaa hiyo, ambaye jina lake limehifadhiwa mwenye umri wa miaka 65, kwa tuhuma za kumnajisi mtoto mdogo wa umri wa miaka tisa, anayesoma darasa la pili, kwa kumlaghai kumpa pipi na shilingi 200.
Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Marko Godfrey Chilya, amekiri kupokea taarifa ya kunajisiwa mtoto huyo na kueleza wanaendelea kumsaka mtuhumiwa huyo kwa udi na uvumba hadi pale atakapopatikana na kumfikisha mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.
Chilya amesema kwa sasa mtuhumiwa huyo inadaiwa ametoroshwa na ndugu zake na kupelekwa kusikojulikana,kufuatia kupata taarifa ya kutafutwa kwake, kutokana na kitendo cha kikatili dhidi ya mtoto asiye na hatia.
Hasidi Ally ni shangazi wa mtoto huyo, ameeleza kwamba alibaini kufanyiwa unyama huo,baada ya kumuona akiwa amekosa raha, huku akiwa anatokwa na harufu isiyo rafiki na alipomhoji akamtaja mtuhumiwa huyo kumfanyia unyama na kumpa pipi na shilingi 200.
Shangazi huyo amesema baada ya kumfikisha Zahanati na kuangaliwa na daktari, alielezwa ampeleke mtoto yule Hospitali ya mkoa kutokana na ukubwa wa tatizo lake.
Chanzo - EATV
Social Plugin