Katika mabadiliko hayo, Askofu Sangu amemteua aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Buhangija Padre Deograthias Ntindiko kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Nyalikungu, ambapo aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Nyalikungu Padre Simon Maneno, ameteuliwa kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Buhangija.
Pia, amemteua aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Kilulu Padre Andrea Mabula kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Wila, huku aliyekuwa Paroko wa Parokia hiyo ya Wila Padre Lwanga Misana akimteua kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Nindo na Afisa utumishi wa Jimbo.
Halikadhalika, amemteua aliyekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Gula Padre Beatus Maduhu kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Mwamapalala, huku aliyekuwa Paroko wa Parokia hiyo Padre Emmanuel Kahabi akiteuliwa kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Maganzo.
Askofu Sangu pia, amemteua aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Maganzo Padre Martine Jilala kuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Sayusayu na mlezi wa wanafunzi wa mwaka wa malezi,ambapo aliyekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Buhangija Padre Michael Kumalija, amemteua kuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John Bariadi.
Wengine ni aliyekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Sayusayu Padre Patrick Ngasa ambaye ameteuliwa kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Kilulu, huku aliyekuwa Paroko msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu John Bariadi Padre Abel Jipili akimteua kuwa Paroko mpya wa Parokia ya Mwanangi.
Aidha askofu Sangu amewatambulisha rasmi wakuu wa vitengo na idara mbalimbali za jimbo ambao ni pamoja na Padre Mathias Mashaka ambaye ni mkuu wa idara ya Uchungaji, Padre Josephat Mahalu ambaye anaendelea kuwa mkuu wa utume wa Walei, Padre Joseph Komanya ambaye anaendelea kuwa mkuu wa idara ya Elimu na Padre Dokta Robert Shija,ambaye ameteuliwa kuwa mkuu mpya wa idara ya Afya.
Wengine ni Padre Anatoly Salawa ambaye ataendelea kuwa mkuu wa idara ya Mawasialiano jimbo, Padre Paschal Kasase ambaye ataongoza idara ya fedha,Mipango na ujenzi akisaidiwa na Padre Injinia Michael Msabila huku Padre Renatus Mashenene akiendelea kuwa mkurugeni wa utume wa Caritas ambaye atashirikiana na Padre Paul Kitaly.
Aidha, askofu Sangu amemtamtangaza Padre Deusdedith Mhula kuendelea kuwa mkurugenzi wa jimbo wa tume ya haki na amani, ambapo Padre Albert Izengo ameteuliwa kuwa mkuu wa idara ya Mahusiano na ushirikiano dini zingine (Ecumenism & Inter Religious Dialogue)
Halikadhalika, amewatangaza Monsinyori Nobert Ngusa kuendelea kuwa mkurugezni wa masuala ya Litrujia jimboni, Padre Deusdedith Mhula kuwa mkuu wa Wakleri,Padre Simon Maneno kuwa Mkurugenzi wa Miito na Padre Paul Kitaly kuwa mlezi mpya wa Watawa.
Askofu Sangu vilevile amewatambulisha wakuu wa vitengo mbalimbali katika kanisa ambapo Padre John Kulwa Kashinje atasimamia kitengo cha Kilimo, Padre Injinia Michael Msabila atasimamia Kitengo cha Ardhi na Ujenzi, Padre Francis Kamani ataendelea kuwa mkuu wa Mashirika ya Kipapa kwa kushirikiana na Padre Peter Mkunya ambapo Padre Paul Nhindilo ataendelea kuwa Hakimu wa mahakama ya kanisa.
Askofu Sangu pia amemteua Padre Emanuel Kahabi kuwa mlezi mpya wa shirika la Watawa la Kijimbo la Mtakatifu Bikra Maria Mama mwenye Huruma, ambapo Sister Sophia Afoa wa Shirika la Marist amemtangaza kuendelea kuwa mkurugenzi wa vijana kwa kushirikiana na Padre Peter Mkunya.
Chanzo - Radio Faraja Fm blog