TANZANIA YANG’ARA UCHAGUZI MKUU WA UMOJA WA WATOA HUDUMA ZA POSTA KUSINI MWA AFRIKA (SAPOA)

Ujumbe wa Tanzania kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa SAPOA Bwana Janras Serame Kotsi (wa pili kulia). Kutoka kushoto ni Mhandisi Kulwa Fifi, Kaimu Meneja wa Biashara mtandao, Bwana Constantine Kasese, Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara, Janras Kotsi (SAPOA) na Elia Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa.
Bwana Constantine Kasese,Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara za Shirika, aliyemwakilisha Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania akimpongeza Bwana Elia Madulesi mara baada ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Utawala ya SAPOA na baadae Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo jijini Cape Town,Afrika ya Kusini wakati wa vika vya SAPOA vinavyoendelea.

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia za Kidijitali wa Afrika ya Kusini Mheshimiwa Phillemon Mapulane (Mb) katika aliyekaa,akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Utawala ya SAPOA. Waliokaa kulia kwake ni Bwana Festus Hangula, Mwnyekiti wa Bodi na kushoto kwake ni Bwana Elia Madulesi, Makamu Mwenyekiti.Waliosimama kutoka kushoto ni Cornelius Ramatlhakwane, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Botswana (Mjumbe), Bibi Nomkhita Mona, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Afrika Kusini(Mjumbe) na Bwana Janras Kotsi Mtendaji Mkuu wa SAPOA

****
Cape Town, South Africa


Tanzania kupitia Shirika la Posta nchini imechaguliwa kuingia kwenye bodi ya Utawala ya Umoja wa Watoa Huduma za Posta Kusini mwa Afrika (SAPOA) kwenye uchaguzi wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa 20 unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Durbanville, ulioanza tarehe 25-28 Julai, 2022, jijini Cape Town, Afrika ya Kusini. 

Katika mkutano huo Bw. Elia P.K.Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania amepata nafasi hiyo ya kuiwakilisha Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Utawala ya Umoja huo, nchini Afrika Kusini.

Uchaguzi huo uliofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Mwaka wa SAPOA, uliohusisha nchi zilizo katika Umoja huo ambao ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Vilevile, katika Bodi hiyo Bw. Madulesi, amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwenye Bodi hiyo, huku nafasi ya Mwenyekiti Ikienda kwa Ndugu Festus Hangula, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Namibia. 

Wengine waliochaguliwa kuingia kwenye Bodi hiyo ni Cornelius Ramatlhakwane, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Botswana, Bibi Nomkhita Mona, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Afrika Kusini na Bibi Elizabeth Mamosehlela Letsoela, Mkurugenzi Mkuu wa Posta ya Lesotho.

Shirika la Posta Tanzania linahudhuria Mkutano Mkuu wa 20 wa Mwaka wa SAPOA na jukwaa la Posta la SAPOA likifanyika sambamba na Mkutano huo. 

Shirika la Posta limewakilishwa na Bw. Constantine Kasese, Kaimu Meneja Mkuu, Uendeshaji wa Biashara ambaye alimuwakilisha Bwana Macrice Mbodo Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kwenye Mkutano huo, Bw. Kulwa Fifi, Kaimu Meneja wa Biashara Mtandao na Bw. Elia P.K. Madulesi, Mkuu wa Mawasiliano na Mambo ya Posta Kimataifa.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
27 Julai, 2022

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post