Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga yakihusisha washiriki 194. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema amefunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na
Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga huku akiwasisitiza
wahitimu hao wa mafunzo kuwa wazalendo na kuepuka kuwa wakali kwa wananchi.
Mafunzo hayo
yaliyodumu kwa siku 21,2022 yamefungwa leo katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY
COM Mjini Shinyanga yakihusisha washiriki 194.
“Nendeni mkamalize kazi, kafundisheni yale
mliyofundishwa. Msiende kupotosha jamii kuhusu sensa ya watu na makazi, nendeni mkafanye kazi kwa uzalendo na umakini mkubwa ili sensa ya watu na
makazi iwe na mafanikio”,amesema Mjema.
“Msiende na
ya kwenu,nendeni mkatumie madodoso mliyofundishwa. Muwe wapole mnapoongea na
wananchi. Usiwe mkali kama mwananchi hafunguki unapomuuliza”,ameongeza Mjema.
Ametumia
fursa hiyo kuwataka viongozi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa elimu ya sensa
ya watu na makazi huku akibainisha kuwa mkoa wa Shinyanga umejipanga kikamilifu
kufanikisha zoezi la sensa ya watu na
makazi Agosti 23,2022.
“Kazi iliyobaki
sasa ni kulipiga debe la sensa hadi kieleweke. Ukiwa na mkeo au mmeo huko nyumbani mwambie kuhusu Sensa,
tuongeze juhudi za kutoa elimu ya sensa na makazi”,amesema.
Mratibu wa
Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Shinyanga,
Eliud Kamendu amesema mafunzo ya Makarani, Wasimamizi wa Maudhui na
wasimamizi wa TEHAMA mkoa wa Shinyanga yaliyofanyika kwa siku 21 yalianza Julai
6,2022 na yatafikia tamati Julai 26,2022 yakiwa na jumla ya washiriki 194 kati
yao makarani 184, wakufunzi 7, mratibu msaidizi wa sense mkoa na mratibu wa sensa
mkoa.
“Mafunzo
haya yalianza kutolewa kwa kufundisha Dodoso la Jamii, Dodoso kuu la sense,
dodoso la makundi maalumu, dodoso la majengo na miongozo mbalimbali ya
wakufunzi, wadhibiti ubora na waratibu wa sensa ngazi ya wilaya. Hali kadhalika
mafunzo haya yalijumuisha kwenda uwandani kujifunza kwa vitendo mambo yote
yaliyofundishwa darasani katika madodoso yote sambamba na kufanya majaribio kwa
makarani”,amesema Kamendu.
“Mafunzo
haya yamefanyika katika ubora wa hali ya juu na timu hii imekuwa timu ya
ushindi ambayo itakwenda kuwafundisha vyema makarani, wasimamizi wa maudhui na
wasimamizi wa TEHAMA ngazi ya wilaya kuanzia Julai 29,2022 hadi Agosti 16,2022
kwa ustadi mkubwa ambao ndiyo watakaokwenda kutekeleza zoezi zima la sensa ya
watu na makazi kwa mwaka 2022”,ameeleza Kamendu.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga yakihusishwa washiriki 194. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akizungumza wakati akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga yakihusisha washiriki 194.

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga yakihusisha washiriki 194. Kulia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga , Elias Masumbuko, kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Sophia Mjema.
Mratibu wa Sensa ya Watu na Makazi Mkoa wa Shinyanga, Eliud Kamendu akitoa taarifa ya mafunzo wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga.

Katibu wa UVCCM Mkoa wa Shinyanga, Raphael Nyandi akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema akifunga mafunzo ya Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Julai 25,2022 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu SHY COM Mjini Shinyanga.
Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.

Viongozi mbalimbali wakiwa ukumbini

Viongozi mbalimbali pamoja na Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Walimu wa Makarani na Wasimamizi wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin