Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RC HAPI ATAKA WAKUFUNZI WA SENSA KUSISITIZA NIDHAMU

Na Shomari Binda - Musoma

WAKUFUNZI wa Sensa ngazi ya mkoa wa Mara wametakiwa kwenda kusisitiza suala la nidhamu kwa makarani watakaosimamia zoezi hilo.


Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mara,Ally Hapi,wakati akifunga mafunzo ya siku 21 kwa wakufunzi 296 wa ngazi ya mkoa.  


Amesema zoezi la Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ni muhimu kwa serikali kupata takwimu sahihi hivyo ni muhimu kuzingatia suala la nidhamu.


Hapi amesema anaamini wakufunzi wa ngazi ya mkoa wamepata elimu na ufahamu wa kutosha na wakaitumia kwenda kufundisha ngazi ya wilaya.


Amesema kila mmoja anapaswa kuzingatia weledi na nidhamu ya kwenda kufanya kazi hiyo na yule asiyekuwa na sifa asipewe kazi ya sensa.


Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwa watu 960 watakaofanya kazi hiyo ndani ya mkoa wa Mara lazima wawe watu sahihi ili zoezi hilo lisiharibike.


"Leo tunafunga mafunzo ngazi ya mkoa lakini kuna zoezi muhimu bado linaendelea ikiwa ni kuisaidia serikali kupata takwimu sahihi.

" Tukawafundishe wote watakaoshiriki zoezi hili suala la nidhamu ni jambo la msingi ili mkoa uweze kufanya vizuri",amesema Hapi.

Kwa upande wao baadhi ya wakufunzi hao wamesema watakwenda kufanya kazi hiyo kadri walivyojifunza kutoka kwa wakufunzi wa kitaifa


Wamesema suala la nidhamu watakwenda kulizingatia ili kupata watu sahihi watakaokwenda kufanya kazi hiyo kwenye kaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com