Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHAKA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO PEMBA,ATAKA WABUNGE,MADIWANI NA WAWAKILISHI WALINDWE


Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka (katikati) akisalimiana na Mwananchi wa jimbo la Gando vsiwani Pemba baada ya kumkabidhi baiskeli ya Kutembelea iliyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo Salim Mussa Omari (wa pili kulia). Shaka amemkabidhi baiskeli hiyo jana na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa.

Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Pemba
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo visiwani Pemba huku akitumia nafasi hiyo kueleza Chama hicho kitaendelea kuwalinda na kutambua mchango wa wabunge,madiwani na wawakilishi ambao wako mstari wa mbele kutekeleza miradi ya maendeleo.

Shaka akiwa katika ziara hiyo iliyoanza jana visiwani humo amepata nafasi ya kukagua miradi ya ujenzi wa madarasa na kisima cha maji safi na salama katika Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya kufuata maji umbali mrefu.

Akiwa katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Salim Mussa Omar na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mariam Thani Juma na kufanyika kwenye Uwanja wa Mpira Kizimbami Shaka amesema utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaofanyika katika jimbo hilo na maeneo mengine yanayoongozwa na wabunge na madiwani wa CCM.

"Utekelezaji wa miradi unaofanywa na viongozi wa CCM unalenga kutekeleza ahadi na kutatua changamoto za wananchi katika huduma za jamii ikiwemo afya, elimu na maji.Niwahakikishie wabunge,madiwani na wawakilishi wanaotokana na CCM kwamba Chama kitaendelea kuwalinda dhidi ya yeyote anayetaka kuwavuruga na kusababisha washindwe kutekeleza majukumu yao.

"Wabunge,madiwani na Wawakilishi wanapaswa kuachwa watekeleze Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba mwanachama yeyote mwenye malengo ya kuomba uongozi asubiri wakati mwafaka unaoruhusiwa kisheria,"amesema Shaka .

Maelezo hayo ya Shaka yalitokana na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Gando kutoa kilio chao mbele ya mkutano huo kuna baadhi ya wanachama wa Chama chao wamekuwa wakiwashika mashati na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu pamoja na miradi ya maendeleo,hivyo kutoa ombi kwa Chama kuangalia namna ya kukomesha hali hiyo.

Awali kabla ya kuhudhuria mkutano huo mapema asubuhi aada ya kuwasili kisiwani Pemba , Shaka alizuru kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Serikali ya Awamu ya Tatu marehemu Dk. Omari Ali Juma, wilayani Chakechake.

Shaka baadae alikwenda kwenye kaburi la aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar marehemu Maalim Seif Sharif Hamad lililopo Kijiji cha Mnyali, Mtambwe wilaya ya Were Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akiwa katika makaburi hayo Shaka ametumia nafasi hiyo kueleza mchango wa viongozi hao ambao enzi za uhai wao wamelitumikia Taifa kwa uadilifu mkubwa na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uzalendo mkubwa.

Aidha amesema wakati Watanzania wakiwa wametimiza miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi vya siasa mchango wa Dk .Omari Ali Juma pamoja na Maalim Seif hautasahaulika kwani walijitoa kwa kiwango kikubwa kuufanikinisha mfumo huo

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akishiriki ujenzi wa kisima cha maji safi na salama katika Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya kufuata maji umbali mrefu.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwa sambamba na Mbunge jimbo la Gando Mhe.Salim Mussa Omari (wa pili kulia) akishiriki ujenzi wa kisima cha maji safi na salama katika Jimbo la Gando, miradi ambayo imewapunguzia adha wananchi ikiwemo ya kufuata maji umbali mrefu.
Mbunge jimbo la Gando Mhe.Salim Mussa Omari akizungumza jambo mbele ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka katika kijiji cha Raha jimboni humo. Ndugu Shaga alikagua mradi huo wa Kisima cha Maji na kushiriki ujenzi wake.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akionesha jambo alipokuwa akikagua moja ya mradi ujenzi wa Vyumba sita vya madarasa ulioanzishwa na Wananchi wenyewe kwa kutoa michango ya fedha na nguvu,sambamba na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na kamati ya maendeleo ya Shehia ya Gando,ndani ya jimbo la Gando.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka akiwasha moja ya gari la kubebea wagonjwa kabla ya kukabidhi kwa wananchi wa Jimbo la Gando. Shaka amekabidhi funguo za gari hilo jana likiwa limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Gando, Salim Mussa Omari .
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya gari la kubebea wagonjwa kwa mmoja ya wananchi wa Jimbo la Gando (wa pili kushoto). Shaka amekabidhi funguo za gari hilo jana likiwa limetolewa na Mbunge wa Jimbo la Gando, Salim Mussa Omari (wa kwanza kushoto) na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akiwasalimia wanacha na wafuasi wa CCM mara baada ya kuwasili katika Ofisi za chama hicho Wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba
Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akipokewa mara baada ya kuwasili katika Ofisi za chama hicho Wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Wete visiwani Pemba wakati wa mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbunge wa Jimbo la Gando Salim Mussa Omari pamoja na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mariam Thani Juma. Mkutano huo umefanyika jana katika Uwanja wa Mpira Kizimbani na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi wa Wilaya ya Wete.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com