Aishi Manula amesaini mkataba mpya na Simba SC hadi 2025
GOLIKIPA namba moja wa Klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania Aishi Manula ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kubaki katika mitaa ya msimbazi kwa muda wa miaka mitatu (3).
Akiwa na Simba Manula amefanikiwa kuchukua makombe manne ya Ligi Kuu Bara, Makombe Mawili ya Azam Sports Federation pamoja na kufanikiwa kutinga mara tatu katika hatua ya Robo Fainali ya Mashindano ya CAF kwa ngazi ya vilabu.
Manula ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri kwa zaidi ya miaka minne akiwa na wekundu hao wa msimbazi ataendelea kubakia msimbazi hadi kufikia mwaka 2025 ambapo mkataba wake utamalizika.
Aishi Manula, Golikipa namba moja wa klabu ya Simba na Timu ya Taifa ya Tanzania
Kulikuwa na fununu za kumhusisha mchezaji huyo kutakiwa na vilabu mbalimbali nje ya nchi kutokana na kuonesha kiwango cha hali ya juu hasa katika michezo ya kimataifa kwa msimu uliopita ambapo klabu yake ya Simba ilifanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Social Plugin