BENKI YA TCB YAWAPA MCHONGO WASTAAFU SHINYANGA KUNUFAIKA NA MAFAO YAO



Afisa wa benki ya TCB kutoka Makao Makuu Yvonne Shoo akizunguma na Wastaafu.
Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza na Wastaafu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

BENKI ya Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TCB) Tawi la Shinyanga, imekutana na Wastaafu Manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia elimu namna ya kunufaika na mafao yao kwa kutumia fursa mbalimbali za kifedha zilizopo katika Benki hiyo.

Elimu hiyo ya kifedha imetolewa leo Julai 6,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.


Meneja wa Benki hiyo ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso, amesema wamekuwa na fursa mbalimbali kwa ajili ya Wastaafu katika Benki hiyo na baadhi yao tayari wameshaanza kunufaika nazo, ndipo wakaona ni vyema wazitangaze fursa hizo kwa wastaafu wengi zaidi ili waneemeke na Mafao yao.

Amesema baadhi ya Wastaafu wamekuwa wakipata fedha za mafao yao, lakini wamekuwa wakishindwa namna ya kuzitumia vizuri na wengine kuishi kufanyia mambo ya anasa, na mwisho wa siku fedha zinakwisha na kubaki hawana kitu.

“Benki ya TCB tumekutana na Wastaafu hapa Shinyanga na kuwatangazia fursa mbalimbali ambazo tunazo kwa ajili yao, ili wazitumie na kunufaika na mafao yao kwa kuziwekeza sehemu salama,”amesema Mataso.

Aidha, ametaja fursa walizo nazo kwa ajili ya Wastaafu, kuwa kuna Akaunti ya Muda Maalumu ambayo Mstaafu atawekeza pesa zake za mafao na kupata asilimia 10 ya faida na kupewa riba hiyo kila Mwezi.

Ametolea mfano kuwa, Mstaafu akiwekeza Sh.Milioni 100 ndani ya mwaka mmoja atapata faida ya Sh.Milioni 10.

Ameitaja Akaunti nyingine ambayo inaitwa Kivulini, ambayo yenye inafunguliwa bure na haina Tozo ya Kadi, na gharama za makato ya kuendeshea Akaunti kila mwezi zimeshushwa kutoa Sh. 1,800 hadi 1,000.

Amefafanua kuwa Akaunti hiyo ya Kivulini pia ina Bima likiwamo Fao la Kifo, ambapo Mteja wao akifiwa na Mke au mme wake au watoto ambao ni tegemezi kwake atapatiwa pole ya Sh.Milioni 2, na kutoa wito kwa Wastaafu wakafungue akaunti hiyo na kutoka kwenye akaunti ya Akiba.

Katika hatua nyingine, amewataka wastaafu hao kuchangamkia fursa za mikopo ndani ya benki hiyo, ambayo ndiyo benki pekee hapa nchini inayotoa mikopo kwa Wastaafu, na riba yake imepunguzwa kutoa asilimia 25 hadi 16 na mikopo hiyo ina bima, ambapo mteja akifariki dunia mkopo wake unafutwa hakuna kudaiwa tena.

Naye Afisa wa Benki hiyo kutoka Makao Makuu Yvonne Shoo, amesema benki hiyo ina mambo mazuri kwa ajili ya wastaafu, ambapo kuna fursa nyingine wameziandaa kwa ajili yao na zipo katika hatua ya majaribio ikiwamo kununua mikopo pamoja na malipo ya awali ya kiinua mgongo (Pension Advance) ambao itakuwa ikitumika kwa njia ya simu za mkononi.

Kwa upande wake Mstaafu David Madata akizungumza kwa niaba ya wenzake, wameipongeza Benki ya TCB kwa kuwajali Wastaafu na kuwapatia elimu ya kifedha na namna ya kutumia vizuri fedha zao za mafao, kupitia fursa zilizopo katika Benki hiyo.

Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza na Wastaafu.

Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza na Wastaafu.

Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akizungumza na Wastaafu.

Afisa wa benki ya TCB kutoka Makao Makuu Yvonne Shoo akizunguma na Wastaafu.

Afisa kutoka Benki ya TCB akizungumza na Wastaafu.

Afisa kutoka Benki ya TCB Grace Gimu akizungumza na Wastaafu.

Mstaafu David Madata akitoa shukrani kwa niaba ya Wastaafu wenzake kupata elimu ya kifedha na fursa za Wastaafu zilizopo ndani ya Benki ya TCB.

Mstaafu Anna Kwilasa akitoa shukrani kupatiwa mafunzo ya kifedha na fursa za Wastaafu zilizopo ndani ya Benki ya TCB.

Wastaafu wakiwa kwenye mafunzo ya kifedha na kutangaziwa fursa mbalimbali za Wastaafu zilizopo katika Benki ya TCB.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Wastaafu wakiendelea kupata elimu.

Afisa kutoka Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Lupiana Daniel, akiwapatia fomu Wastaafu za kufungua akaunti za Kivulini, mara baada ya kumaliza kupewa elimu ya kifedha na kutangaziwa fursa za Wastaafu zilizopo ndani ya Benki hiyo.

Wazee wakiendelea kumiminika ndani ya Benki ya TCB kuchangamkia fursa mbalimbali za Wastaafu ambazo wametangaziwa zilizopo katika Benki hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post