TWITTER KUMSHTAKI BILIONEA NAMBA MOJA DUNIANI BAADA YA KUZINGUA 'KUJITOA' DILI


Parag Agrawal Mkurugenzi wa Kampuni ya Twitter

BODI ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Twitter wamesema wanatarajia kumfungulia kesi Mahakamani Bilionea na Tajiri namba moja duniani Elon Musk kutokana na uamuzi wake kujitoa kwenye dili la kuinunua Kampuni hiyo.


Hivi karibuni Musk ameishutumu Twiiter kwa kutoa taarifa za uongo juu ya uwepo wa akaunti feki kwenye mtandao huo, sababu iliyopelekea bilionea huyo kubadili maamuzi yake ya kuwekeza zaidi ya dola bilioni 44 kuinunua Kampuni hiyo.

Elon Musk Bilionea namba moja Duniani

Musk (51) alikubali kutoa kiasi cha dola Bilioni 1 ambayo ni sawa na Trilioni 2 na bilioni 332 za kitanzania kama fidia ya kuvunja mkataba huo lakini Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Paraga Agrawal amedhamiria kulipeleka suala hilo Mahakamani na kulazimisha dili hilo likamilike.


Bilionea huyo ametahadharishwa kuwa kwa kitendo cha maamuzi yake ya kususia kuinunua Kampuni hiyo kinaweza kumgharimu kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa hajathibitisha ni kwa kiasi gani Twitter ina akaunti feki lakini pia sababu hiyo imetajwa kutokuwa na mashiko hadi kusababisha kukwama kwa ukamilikaji wa dili hilo.
Elon Musk ametahadharishwa juu ya maamuzi yake ya kughairi kuinunua Twitter

Tayari Twitter imeajiri kampuni ya Kisheria ya Wachtell, Lipton, Rosen na Katz kutoka jijini New York Marekani kujiandaa tayari kwa ajili ya kupeleka shauri Mahakamani dhidi ya Bilionea Elon Musk.


Aidha Musk ametahadharishwa kuwa ipo hatari kubwa ya Kampuni hiyo kufirisika taratibu na hatimaye kufa kabisa kutokana na kuwa na hatari ya kupokelewa vibaya na wateja kama Musk atakamlisha dili la kuinunua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post