Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AFARIKI DUNIA AKISHINDANA KUNYWA POMBE KALI NA WENZAKE



MWANAUME anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 hadi 30, amefariki dunia baada ya kumaliza chupa nzima ya pombe kali ya Jagermeister katika mashindano ya kunywa pombe, yaliyofanyika katika Mtaa wa Mashamba, Limpopo nchini Afrika Kusini.

Mkuu wa Polisi wa Limpopo, Motlafela Mojapelo amesema kijana huyo na wenzake walikuwa kwenye mashindano ya kunywa pombe kali, ambapo mshindi aliahidiwa kupewa kiasi cha randi 200 za Afrika Kusini (takribani shilingi 27,000 za Kitanzania).

Akazidi kueleza kuwa marehemu alifanikiwa kumaliza chupa nzima ya pombe hiyo kali, lakini muda mfupi baadaye alianguka na kupoteza fahamu na baadaye kupoteza maisha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com