Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Stella Kahwa (wa tatu kushot) akiwa pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Taasisi hiyo katika picha ya pamoja kwenye banda lao katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud S. Kigahe (kushoto) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa mara baada ya kutembelea banda la WMA katika Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (TWA) Bi. Stella Kahwa (wa tatu kulia) akizungumza na Moja ya Mtangazaji wa kipindi Maalum cha Sabasaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea JijiniDar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (TWA) Bi. Stella Kahwa (wa kwanza kushoto) akifurahia jambo na baadhi ya watumishi wa Taasisi hiyo.
Na: Mwandishi wetu, DAR
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) Stella Kahwa amesema kuwa Taasisi hiyo imeainisha vituo zaidi ya elfu tano nchi nzima kwaajili ya kufanya ukaguzi ili kuendelea kuhakikisha mtanzania anapata Bidhaa iliyo katika ujazo na vipimo vinavyostahili sambamba na kuendelea kuwabaini wafanyabiashara wanaofanya udanganyifu.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Stella Kahwa katika mahojiano na waandishi wa habari Julai 3,2022 kwenye Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Kahwa amesema kuwa kuwepo kwa vituo hivyo kumeleta matokeo chanya na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto mbalinbali zilizokuwa zikiwakabili walaji na kwamba kwa sasa wengi wao wanafanya biashara zao kwa kufuata taratibu zilizopo.
"Kwa sasa Changamoto hii imepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunapoenda kufanya kaguzi hatukutani na waliokiuka taratibu hata wale wanaopigwa faini wamepungua sana hadi kufikia asilimia 80 na 85" amesema.
Aidha ameendeleakutoa mwito kwa wafanyabiashara na walaji kwa ujumla kuendelea kufuata taratibu zilizopo ili kila mmoja aweze kunufaika.
Pia amewakaribisha wananchi wote hususani wafanya Biashara kufika kwenye Maonesho ya sabasaba na kutembelea Banda lao ili kujifunza na kufahamu namna Taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.
"Nawaambia wafanyabiashira waje hapa sabasaba wajionee namna ambavyo wakala wa vipimo inavyofanyakazi, Wakala wa Vipimo iko Juu hivi sasa" alihitimisha Kahwa.
Kwa upande wake Afisa Vipimo Mkuu WMA, Bw.Gaspar Matiku amesema kuwa kwa sasa WMA imejipanga kuhakiki vipimo kwenye gari ndogo za biashara (tax) kwa kufunga tax meter ambazo zitasaidia kufahamu mteja ametembea kwa umbali fulani na kuweza kulipa fedha halali ambayo inalingana na umbali aliotembea.
Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kujua umbali na fedha ambayo inatakiwa kulipwa na mteja kutokana na umbali uliotumika.
“Biashara ya Tax imekuwa kubwa na inatumika, sasa badala ya mtu kutamkiwa kwamba unatoka hapa ninakwenda sehemu fulani, huyu anakumbia utanipa elfu 20 na mwingine anakuambia utanipa elfu 30 kwa hiyo hakuna usawa kwenye hiyo ruti” Amesema.
Social Plugin