Mfano wa simu iliyovunja kioo
Maafisa wa polisi Jimbo la Delta nchini Nigeria wamemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 23, Godspower Adegheji, kwa madai ya kumuua mpenziwe katika eneo la Ozoro jimboni humo.
Ilibainika kuwa mshukiwa alimpiga Gift Oloku, 22, kwa panga baada ya kumvunjia kimakosa kioo cha simu yake aina ya IPhone 11 pro max yake Jumamosi, Julai 16, 2022.
Msemaji wa mtoaji amri, Bright Edafe, katika taarifa yake Jumapili, alisema matatizo yalianza baada ya mshukiwa kumhoji marehemu kwanini alikwenda nje kwenye mtoko bila kumwambia.
Inasemekana alimshutumu kwa kutokuwa mwaminifu, jambo ambalo lilisababisha ugomvi, na katika harakati hizo alivunja simu yake kimakosa. Mshukiwa huyo, baada ya hapo, alidaiwa kumkatakata marehemu kwa panga hadi kupelekea umauti na baadae kufariki
Social Plugin