Na Mwandishi wetu, Mbeya
Chama Cha Mapinduzi kimesema licha ya Rais samia suluhu Hassan huzungumza polepole lakini vitendo vyake katika utekelezaji wa sera za maendeleo zimekuwa motomoto.
Pia, serikali yake kwa muda mfupi imeaminika na kuheshimika kikanda na kimataifa.
Matamshi hayo yametamkwa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana alipokuwa katika Manispaa ya jiji la Mbeya.
Kinana alisema Rais Samia amekuwa kiongozi wa mfano ambaye kwa kipindi kifupi cha mwaka mmoja amekubalika katika medani za kidiplomasia huku akiaminiwa na taasisi za kimataifa.
Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, alisema serikali yake imekuwa ikitekeleza wajibu hatua kwa hatua na kuimarika kwa huduma za jamii.
"Rais Samia kiongozi mchapakazi asiye na majivuno. Kila uendapo utakutana na maendeleo ambayo hayakutegemewa yatokee haraka. Anazungumza polepole lakini vitendo ni vizito" Alisema Kinana.
Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti alisema uongozi bora hupimaa kwa kutoa matokeo chanya ambayo kwa bahati nzuei kila sekta imepatiwa fedha za kufanikisha miradi ya maendeleo.
"Kila eneo limegushwa katika maendeleo. Sekta za Maji,Afya ,elimu zimspatiwa fedha kusukuma mbele kwa muktadha wa kupunguza kero na kumaliza changamoto sugu "Alisema Kinana
Social Plugin