Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI AKIJISAIDIA KWENYE KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI



Mkazi wa Kijiji cha Orkine, wilayani Kiteto mkoani Manyara, Nanaa Mepukori (54) amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kujeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri na watu wasiojulikana.


Tukio la mwanaume huyo kukatwa nyeti lilitokea Juni 28, 2022 usiku ambapo inadaiwa kuwa alikuwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji na alipotoka nje kujisaidia akakutana na watu hao na kumkata kwa kutumia kisu.

Mtoto wa mzee huyo, Leyaseki Mepugori (26) akizungumza akiwa hospitali ameeleza kuwa alimkuta baba yake akiwa anavuja damu baada ya kufanyiwa ukatili huo.

 Chanzo - Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com