Mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani ameushangaza ulimwengu baada ya kukiri kujiandaa kwa safari yake ya mwisho duniani kwa kujiundia jeneza ambalo kabla hajafa analitumia kama kabrasha la kuweka vitabu.
Katika hadithi moja ambayo imechapishwa kwenye jarida la Marekani, mwanamke huyo kwa jina Leona Oceania mweney umri wa miaka 52 alisema kwamba yeye aliamua kuanza kuitayarisha safari ya mazishi yake mapema na kuamua kabla siku hiyo haijafika, jeneza hilo liwe linatumika kuwekea vitabu vyake likisubiri shughuli muhimu ya kumzika.
Mwanmke huyo alisema na jarida hilo kwa kusema kwamba hata marafiki wanaomtembelea huwa kila mara wanastaajabu na kuhakikisha kujua kilichoko ndani na kukuta vitabu, ila pia akasema anaamini siku moja tu hivyo vitabu vitatolewa vyote ili kutengeneza nafasi ya kumzika yeye.
“Aliliambia Wall Street Journal kwamba wageni "huwa wanaiangalia" lakini wachache wanakisia kuwa rafu siku moja zitaondolewa ili kutoa nafasi kwa Oceania anapolazwa na kuzikwa kwenye rafu ya vitabu vyake vya nyumbani.
“Kifo kimenishangaza siku zote. Sifikirii kwa njia ya ajabu,” alieleza wanahabari waliojikita sehemu moja kwa mshagao mkubwa.
Jarida hilo lilisema kwamba mwanamke huyo alikuwa anaonekana mwenye furaha kubwa na hawakuamini mbona alikuwa anafikiria kifo chake muda wote akiwa nyumbani kwake kuangalia lile jeneza kila mara na kuwaza tu kwamba vitabu vilivyomo vinamshikilia nafasi kwa muda tu usiojulikana.
Kulingana na taarifa kwenye jarida hilo, Oceania hufanya kazi kama msimamizi katika idara ya kazi ya umma ya manispaa na anajiongeza kama mwongozaji wa mazishi ya nyumbani, mfanyakazi wa kujitolea wa hospitali na msemaji wa umma juu ya sanaa ya kufa vizuri.
Humu nchini, visa vya watu kujinunulia majeneza na wengine kujichimbia makaburi yao huku wakiandika nyaraka zenye utashi mwingi kutoa maagizo ya jinsi msiba wao utakavyoendeshwa ni nadra mno na vinapotokea huwa ni mambo ya kustaajabisha sana katika jamii, baadhi wakisema sharti tambiko lifanyike ili kukemea mawazo na fikira kama hizo kwani kulingana na mila zingine, mtu hafai kuzungumzia kifo chake, achia mbali hata kuratibu.
Social Plugin