KANISA LATOA VYETI VYA UBIKRA KWA MABINTI BAADA YA KUWAPIMA


Kanisa moja la Afrika Kusini linafanya vipimo vya ubikira kwa waumini wa kike wa kanisa hilo wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Inaripotiwa kwamba Kanisa la Nazareth Baptist mjini Durban, Afrika Kusini lilianza mazoezi hayo ili kuwahimiza wanawake wachanga kanisani kutunza ubikira wao.

Inasemekana kuwa ni zoezi la kila mwaka ambalo hufanyika katikati ya mwaka na 'Cheti cha Ubikira' hutolewa kwa wale wanaofaulu mtihani na alama nyeupe inapakwa kwenye vipaji vyao.

Vyeti hivyo ni halali kwa mwaka mmoja tu na wanawake wanatarajiwa kufanya kipimo kingine katika mwaka unaofuata.

Kipimo cha ubikira mwaka wa 2022/2023 kilifanywa na kanisa hilo siku ya Jumanne, Julai 6,2022 na wanawake waliofaulu walipewa cheti kama kawaida.

Cheti hicho kilitiwa saini na kiongozi wa kanisa hilo na mtaalamu aliyekagua ubikira wao.

Je ubikra unapimwa vipi?

Kipimo cha ubikra hufanywa kutambua iwapo mwanamke amewahi kushiriki ngono na mwanamume au la.

 Bikra huaminika kama ndio kipimo cha usafi na tabia nzuri kabla ya ndoa.

 Nchini Afrika Kusini, wanawake hupimwa ubikra kabla ya kupelekwa kwa masomo nje ya nchi na pia kuzuia maambukizi vya virusi vya ukimwi ambayo yako juu sana nchini humo.

 Ubikra hupimwa na kipimo ambacho kitaalamu kinafamika kama two fingers virginity test ambapo mara nyingi madaktari hutumika kufanya vipimo hivyo. 

Wakati wa vipimo hivyo, vidole viwili huingizwa ndani ya uke kuangalia ngozi laini kwa jina hymen ambayo inaaminika huchanika mwanamke anaposhiriki ngono kwa mara ya kwanza.

Ngozi hiyo ikipatikana haipo, basi mwanamke huyo si bikra na ikipatikana basi ni bikra. 

Njia nyingine ambayo jamii nyingi hutumia ni kuweka shuka nyeupe kwenye kitanda na damu ikitoka wakati wa ngono, basi mwanamke huyo ni bikra. 

Hata hivyo, si rahisi kupima iwapo mwanamume ni bikra kwani wote wako sawa kimaumbile wakiwa bikra au la.

Via >> Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post