Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari katika ziara ya kazi kwenye ufunguzi wa Maonesho ya 46 ya Viwanda na Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam, Tarehe 3 Julai,2022.
Dkt. Bakari ameeleza lengo la TCRA katika kuendelea kutoa fursa kwa wabunifu mbalimbali wa TEHAMA kutumia bure rasilimali za mawasiliano kwa ajili ya kukamilisha majaribio yao.
Pia amewahimiza wananchi kufika katika viwanja vya Sabasaba na kutembelea banda la TCRA lililopo jirani na 'roundabout' iliyomo ndani ya viwanja vya Maonesho ili kupata elimu na msaada kuhusu huduma na bidhaa za mawasiliano.
KAULI MBIU: “Tanzania, mahali sahihi pa Biashara na Uwekezaji.”
Social Plugin