Meneja Masoko TANESCO Mwl. Mussa Kassim
Wakazi wa Mkoa wa Tabora wamefurahishwa na hatua ya kuanza kufaidika na huduma mpya ya kupata huduma za kwa njia ya kidigitali ya shirika la umeme nchini TANESCO ambayo imeanza kutumika hivi karibuni inayojulikana kama Ni- konekt.
Meneja masoko wa shirika hilo kutoka Makao makuu Dodoma Mwl. Mussa Kassim akiwa mkoani Tabora alielezea huduma hiyo kuwa ni rahisi na inapatikana kupitia kompyuta na simu za kiganjani ambapo mwananchi anaweza kuomba na kunganishiwa huduma ya umeme bila kufika katika ofisi za shirika .
Pia amesema huduma hiyo ni msaada mkubwa kwa wananchi ambao wakati mwingine wamekuwa wakikutana na matapeli katika mazingira ya kutafuta huduma ya kuunganishiwa umeme.
Mmoja kati ya wanufaika wa huduma hiyo mkoani Tabora Lucas Shilima wakati alipotembelewa nyumbani kwake alisema alitumia huduma ya Ni- konekt na kuunganishiwa umeme nyumbani kwake ndani ya muda wa siku mbili.
Katika hatua nyingine meneja wa TANESCO mkoa wa Tabora mhandisi Hadija Mabrouck amesema shirika linaendelea kuboresha na kujenga miundo mbinu mipya ya huduma ya umeme katika Mkoa wa Tabora na hivyo huduma ya umeme ni ya uhakika huku akiomba wawekezaji katika mkoa huo kutokuwa na wasisi kuhusu huduma ya umeme.