Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATOTO 285 WANAOISHI MAZINGIRA HATARISHI RORYA KUNUFAIKA NA SARE ZA SHULE

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rorya Gerald Ng'ong'a akikabidhi msaada wa kwa mmoja wa watoto
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rorya Gerald Ng'ong'a akizungumza
Mratibu wa Mradi wa Achieve Charles Ally kutoka RAFIKI SDO akielezea juu ya Mradi huo.
Afisa ustawi wa jamij Halmashauri ya Rorya Saul Charles akieleza Hali halisi ya Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Na Frankius Cleophace Rorya.


Watoto 285 katika Halmashauri ya wilaya ya Rorya Mkoani Mara kutoka katika shule za msingi wanatarajia kunufaika na sare za shule kutoka shirika la RAFIKI SDO.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi sare hizo mratibu wa mradi wa Achieve kutoka shirika la RAFIKI SDO Charles Ally amesema kuwa mradi huo umelenga kuboresha Ustawi na Afya kwa watoto ambao wanaishi mazingira hatarishi.

Ally alisema kuwa mradi huo umelenga kuboresha Ustawi wa watoto wanaioshi mazingira hatarishi pamoja na watoto ambao wanalea wazazi wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi lengo ni kuhakikisha watoto wanaenda shule nakupata haki zao za msingi.

“Katika mkoa wa Mara tunatekeleza huu mradi wa Achieve katika Halmashauri ya Bunda, Rorya na Manispaa ya Musoma” ,alisema Ally.

Ally aliongeza kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya malezi na makuzi ya awali ya mtoto ambapo malezi hayo ni msingi bora kwa watoto hususani kuanzia miaka 0-8.

Suala la malezi ni jukumu la wazazi wawili baina ya Baba na Mama hivyo jitiada zinazofanywa na mashirika mbalimbali kwa kushirikiana na serikali wenda ukawa mwarobaini kwa watoto.

Malezi Jumuishi ya Awali yanatilia mkazo utendaji unaoendana na muktadha na huduma zitolewazo kuhakikisha watoto wadogo wanastawi na kuhuishwa, neno MMMAM ni pana zaidi, likishughulikia nyanja jumuishi za maendeleo ya mtoto ambazo zinahitaji kushughulikiwa kupitia huduma za malezi jumuishi ya awali.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa jamii Halmashauri ya wilaya ya Rorya Saul Charles alisema kuwa Jumla ya watoto 13,441 wanaishi katika mazingira hatarishi ambapo watoto 6000 wanaishi katika mazingira hatarishi zaidi na pia hawana wazazi.

Hivyo Afisa Ustawi amelipongeza shirika la RAFIKI SDO kwa kutoa msaada wa sare za shule kwa wanafunzi 285 katika Halmashauri ya wilaya ya Rorya nakuomba taasisi nyingine kuencelea kujitoa kwa ajili ya kusaidia makundi yenye mahitaji.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rorya Gerald Ng’ong’a alisistiza wazazi sasa kupeleka watoto shule ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu.

Kaimu Afisa Elimu Msingi Maiga Maiga alisema kuwa wazazi waondikane na tabia ya kupeleka watoto kuchunga Mifugo badala yake wawapeleke shule ili wapatiwe elimu ili kuwasaidia badae wazazi wao.


Aidha wazazi na walezi wawatotowaliopatiwa msaada huo wamedai kuwa sasa watasisitiza watoto wao kwenda shule kwani changamoto kubwa ilikuwa mavazi pamoja na vifaa vya shule.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com