Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Jonson akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani.
Na Shinyanga Press club Blog
Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga utaanza kuilipa halmashauri hiyo kiasi cha Sh Bilion 1.2 kuanzia mwaka wa fedha ulioanza Julai Mosi 2022/2023 kama tozo ya huduma ili kusaidia utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Hayo yameelezwa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Kishapu na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Emmanuel Jonson wakati akiwasilisha mpango wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo kupitia fedha zinazotolewa na mgodi wa Mwadui.
Mkurugenzi Jonson amesema mgodi huo una umri wa miaka 80 lakini licha ya kufanya shughuli za uzalishaji, matokeo yake kwa wananchi hayaonekani na ndiyo sababu iliyofanya wakae kikao na uongozi wa mgodi huo pamoja na serikali na kufikia muafaka ambao umezaa matunda kwa kuanza kutoa fedha hizo.
“Awali mgodi huo ulikuwa unatoa fedha kiasi cha Sh Milioni 150 lakini sasa baada ya mazungumzo wamekubaliana mgodi utaanza kulipa fedha kwa asilimia 0.7 ambayo ni wastani wa Bilioni 1.2, fedha ambazo zitakwenda kutekeleza miradi ya maendeleo”, amesema Mkurugenzi.
Amesema tayari mpango wa utekelezaji wa miradi umeandaliwa ikiwemo miradi itakayotekelezwa kwa fedha hizo kupitia sekta mbalimbali hatua ambayo itasaidia kutatua changamoto kwa wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo kwa kuwanufaisha moja kwa moja.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Wiliam Jijimya amesema wataendelea kusimamia rasilimali zote za halmashauri hiyo ili ziweze kuwanufaisha wananchi na kueleza kuwa haikuwa kazi ndogo kufikia mafanikio makubwa yaliyoanza kuonekana kwenye halmashauri hiyo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo amesema hatua hiyo inatokana na utekelezaji wa sheria mpya ya Wizara ya madini katika kutoa huduma inatekelezwa na kila mwekezaji ili matokeo yaweze kuonekana hasa kwenye maeneo ya mzunguko zinapofanyika shughuli hizo kwa kuwa ndiyo wanaoathirika .
Amesema fedha hizo Sh Bilion 1.2 zinaweza kuongezeka zaidi kadri uzalishaji utakavyoongezeka,huku akiwaomba madiwani kwenda kusimamia vizuri miradi itakayotekelezwa ili kuleta tija kwa jamii na kuonyesha mafanikio yaliyopatikana kutokana na kuwa na mgodi huo.
Kwa upande wake Mkuu Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewapongeza madiwani,mbunge na watumishi wa halmashauri kwa kufanya kazi kama timu jambo ambalo limewezesha kufikia mafanikio makubwa ikiwemo kuanza kupata fedha hizo kutoka mgodi wa Mwadui.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akifafanua jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Kishapu
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Underson Mandia akiwashukuru madiwani kwa kumchagua tena kwa mara nyingine kwa kumpa kura zote za ndiyo kutumikia wadhifa huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani
Mkaguzi wa ndani wa serikali za Mitaa Shinyanga Marwa Magere akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani,ambapo amesisitiza suala la kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Baraza la madiwani Baraza la madiwani likiendelea
Baraza la madiwani likiendelea
Diwani wa Kata ya Sekebugolo Fredirnand Mpogomi akiwasilisha taarifa
Diwani Richard Dominick wa Kata ya Talaga akiwasilisha taarifa ya kamati ya elimu,afya na maji
Diwani Helena Baraza akiwasilisha taarifa ya kamati
ya kudhibiti Ukimwi.
Baraza la madiwani likiendelea