Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJINA YA MASHEMASI WANAOPEWA UPADRE JIMBO LA SHINYANGA





ASKOFU wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, Alhamisi wiki hii Julai 28,2022 atawapa daraja takatifu la Upadre Mashemasi watano.

Mashemasi hao ni Emmanuel Kimambo wa Parokia teule ya Shishiyu iliyopo wilayani Maswa mkoani Simiyu, Emmanuel Gembuya wa Parokia ya Buhangija katika Manispaa ya Shinyanga,Paul Mahona wa Parokia ya Wila wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Simon Lutamula wa Parokia ya Mwamapalala wilayani Itilima mkoani Simiyu na Elias Vumba wa Shirika la Ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisco (Wakapuchini)

Misa ya Upadrisho itatanguliwa na ibada ya Masifu ya jioni, ambayo itafanyika Jumatano kuanzia saa 11:00 jioni, katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya utolewaji wa daraja la Upadre.

Misa ya Upadrisho,itaanza saa 4:00 asubuhi katika Kanisa kuu la Ngokolo, na itahudhuriwa na Mapadre,Watawa na Waamini kutoka sehemu mbalimbali za ndani na nje ya jimbo.

Chanzo - Radio Faraja fm blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com