Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHUMA YA UVCCM 'CHIEF MAKWAIYA' AJITOSA KUGOMBEA UENYEKITI SHINYANGA MJINI


CHIEF Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.
 CHIEF Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHIEF Fravian Patrick Makwaiya aliyekuwa Afisa Masoko wa Kampuni ya Jambo Food Products ya mkoani Shinyanga, amechukua na kuirejesha kwa wakati fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini.

Amechukua Fomu hiyo leo Julai 10 ,2022 katika Ofisi za (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini na kuirejesha.

Akizungumza wakati wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu hiyo, amesema Umoja huo wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilaya ya Shinyanga Mjini, unahitaji kijana makini, mwenye ushawishi ndani ya Chama na Serikali, na mwenye kuziishi changamoto za vijana na kuzitatua kwa wakati, sifa ambazo yeye anazo.

Makwaiya almaarufu kwa jina la Chuma cha UVCCM, ameongeza sifa zingine ni kusimamia ajenda za vijana kwenye vikao na nje ya vikao, ili aweze kuleta maendeleo ndani ya umoja wa vijana.

"Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga mjini, unahitaji kuwa na Mwenyekiti Mchapakazi na Mwaminifu kama mimi Makwaiya na siyo kijana asiyeweza kutatua shida za vijana," amesema Chief Makwaiya.

Aidha, amesema kutokana uzoefu wake wa uongozi alionao ndani ya Chama na Serikali, na amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi ndiyo sababu iliyomsukuma kugombea nafasi hiyo ya Uenyekiti UVCCM wilaya ya Shinyanga, ili kuleta maendeleo ndani ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula, amesema mpaka sasa waliochukua Fomu kugombea nafasi ya Uenyekiti (UVCCM) wilayani humo wamefika 10.

 CHIEF; Fravian Patrick Makwaiya (kushoto) akikabidhi Fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM wilaya ya Shinyanga, (kulia) ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini Naibu Katalambula akipokea Fomu hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com