Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ATUPWA JELA KWA KUTUKANA MPENZI WAKE NA POLISI WALIOINGILIA


Raia mmoja wa taifa la Nigeria atatumikia kifungo cha siku 30 gerezani iwapo atashindwa kulipa shilingi elfu kumi kwa makosa kumporomoshea matusi mpenzi wake na maafisa wa polisi walioingilia kumwokoa binti huyo.

David Olaydaju alipewa adhabu hiyo na Hakimu Mkuu Mkaazi wa Mahakama ya Kibera Philip Mutua baada ya kukiri makossa ya kusababisha usumbufu wenye uwezo wa kutatiza Amani.

 Olaydaju alitekeleza makossa hayo eneo la Gathondeki mtaani Dagoretti katika Kaunti ya Nairobi mnamo Alhamisi, Julai 14,2022 ambapo alimporomoshea matusi Edith Wachiria akitishia kumpiga.

Raia huyo wa kigeni alianza kumtukana mlalamishi na majirani wake katika makaazi ya Hill View akitishia kumpiga, dada huyo akikimbilia kwa walinzi waliomshauri kupiga ripoti kwa polisi.

Olaydaju alimfuata akielekea katika kituo cha polisi na kumfanya kukimbilia katika mgahawa uliokuwa karibu kwa usalama. 

Mtuhumiwa alimfuata hadi kwenye mgahawa huo ambako alizua kioja na kumtukana kila mmoja aliyekuwepo wakiwemo maafisa wa polisi waliokuwa wakifurahia mlo wao.

Mahakama ilielezwa kuwa maafisa wa polisi waliingilia lakini Olaydaju aliendelea na vioja na matusi na kuwafanya maafisa hadi kumtia mbaroni.

 Walipeleka katika kituo cha polisi cha Kabete na kumwandikia mashtaka ya mienendo ya kukosea wengine na kusababisha usumbufu. 

Olaydaju alisema kuwa alikuwa amekasirishwa na hatua ya mpenzi wake kumfungia katika nyumba hiyo kwa saa kadhaa na kuomba mahakama kumhurumia akielezea kukubali kukosa.

Via Tuko NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com