Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),Theobald Sabi akiwa ndani ya tawi la benki akihudumia wateja,kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),Theobald Sabi akizungumza ndani ya tawi la benki hiyo kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa yaMkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),Theobald Sabi akizungumza ndani ya tawi la benki na watendaji wake,kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
*************
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC),Theobald Sabi,amesema benki hiyo inaendelea kushirikiana na wajasiriamali ili kukuza uchumi wa taifa kwa kuwapa elimu na mafunzo ya namna ya kutoa huduma bora kuwapatia mitaji ili waweze kushindana katika soko. Akizungumza katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaaam,Sabi ameeleza kuwa wao kama taasisi ya kifedha wanashirikiana na wajasiriamali kwa kuhakikisha wanapata nafasi ya kutangaza biashara zao.
"Sisi kama benki tunasisitiza sehemu ya maonyesho yetu,tunashirikiana na wafanyabiashara kutangaza biashara zao na katika banda hili tumewapa nafasi za kuweka bidhaa zao,ambazo wanazalisha hapa nchini na sisi kama taasisi ya fedha tunashirikiana na wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kama mitaji kuendeleza shughuli zao"alisema Sabi
Sabi ameeleza kuwa biashara ya kisasa inahitaji ujuzi na matumizi ya teknolojia katika uzalishaji,benki hiyo inalitambua hilo na inaendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali washindane katika soko katika bara la Afrika.
Social Plugin