Simon Jogwe Mfanyakazi wa NMB aliyepoteza watoto wawili kwa mpigo katika ajali ya gari la King David
MFANYAKAZI wa Benki ya NMB Mkoani Mtwara, Simon Jogwe ni miongoni mwa wazazi waliopoteza watoto katika ajali ya gari iliyotokea leo Kata ya Magegeni, Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Jogwe amepoteza watoto wa pekee wawili Johari Simon miaka 7 na Emmanuel Simon miaka 5, ambao wote walikuwa ni wanafunzi wa shule ya msingi King David.
Ajali hiyo iliyohusisha gari la shule hiyo (King David Primary School) imeua watu 10, wakiwemo wanafunzi nane, dereva na mama mmoja ambaye aliomba lift katika gari hiyo.
Kwa mujibu taarifa ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Hamad Nyembea, wanafunzi watano wasichana na watatu wavulana ndiyo waliopoteza maisha.
Social Plugin