Kabla ya kuchukua Uamuzi wa Kugombea Uenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Bwanku M Bwanku amefanya kazi Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jijini Dodoma akiwa kama Afisa kwenye Kitengo cha TEHAMA na MAWASILIANO- Makao Makuu alikohudumu na kuwa Moja ya nguzo imara kwa kushirikiana na wengine kusemea CCM na Sera zake, kueleza umma mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya CCM na Viongozi wake Wakuu na wote Nchi nzima.
Pia, Kijana Bwanku M Bwanku, alikuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Uchaguzi Cha Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma kilichoratibu na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa CCM wa Rais, Wabunge na Madiwani 2020 na kwa kushirikiana na Wana- CCM wenzake Nchi nzima kufanikisha ushindi mkubwa na wa Kihistoria wa CCM wa asilimia 84 ambao haukuwahi kupatikana toka mfumo wa Vyama vingi urejee 1992 na kufanyika kwa Uchaguzi wa kwanza wa Vyama vingi baada ya kurejea Mwaka 1995.
Bwanku M Bwanku ni Mwandishi wa Habari na Mchambuzi mkubwa sana wa Masuala mbalimbali ya Kisiasa, Kiuchumi, Maendeleo, Kijamii na kadhalika anayefanya kazi na kuchangia Mijadala na Uandishi wa Makala na Habari kwenye Magazeti mengi sana Tanzania na Vyombo vya Habari vikubwa vya Kitaifa.
Bwanku, amekuwa Mtanzania pekee anayeandikia na kuchangia Habari na Makala kwenye Magazeti mengi sana Nchini Tanzania kuliko Mtanzania yeyote yule. Mpaka sasa Bwanku amekuwa akiandikia na kuchangia Makala na Habari kwenye Magazeti ya TANZANIA LEO, MAJIRA, MZALENDO, HOJA, LAJIJI, UHURU, HABARI LEO na Magazeti mengine mengi sana.
Bwanku M Bwanku amekuwa Mwanamapinduzi ya Maendeleo hasa kwenye Mikoa ya Kusini (Mtwara na Lindi) ambapo mara nyingi sana amekuwa akishiriki kwenye masuala mbalimbali ya kusukuma Maendeleo yake. Mwaka 2019 alikuwa na Kampeni yake kubwa sana ya Kuhamasisha Elimu kwa mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuinua hali ya Elimu kwa Mikoa hiyo na kuongeza ufaulu ambapo aliandika mpaka Kitabu chake Maalum cha kuhamasishia Elimu- Kusini kwa lengo la kuhamasisha umma wa Kusini kuanzia kwa Wazazi, Wanafunzi, Wananchi na Wadau wengine wote kuwekeza na kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye Elimu.
Kijana Bwanku M Bwanku amehitimu Masomo yake ya Elimu ya Juu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alikopata Shahada (Degree) yake ya Sayansi ya Siasa na Utumishi wa Umma kwa maana Political Science and Public Administration (BA- PSPA)
Akiwa Chuo Kikuu Ndugu Bwanku M Bwanku alikuwa Kijana mahiri sana aliyesaidia sana kwa kushirikiana na Wanachama wengine wa CCM kujenga Chama ndani na Nje ya Chuo kabla ya kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utawala Bora.
Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi (MTWALISO) wanaosoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM-CHSS & CBSL) na nyadhifa nyingine nyingi kwenye masuala ya Hamasa ndani ya Chama na kujitolea kwa ajili ya Ujenzi wa CCM.