Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amefungua mafunzo ya Sheria ya Manunuzi kwa Bodi ya Uzabuni na Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria. Mafunzo haya yameaza leo tarehe 6-9 Julai, 2022 Jijini Dar es salaam.
Dkt. Ndumbaro amesema mafunzo hayo yaangalie na kuzingatia maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ili kuboresha mfumo wa manunuzi na kuondoa urasimu
"Kama wataalam tutafute fomula itakayotupa mfumo wenye uwazi, thamani ya pesa, ubora wa bidhaa na huduma na kuondoa mianya ya rushwa pasipo kuwepo kwa urasimu" amesema Dkt. Ndumbaro
Social Plugin