Msanii William Lyimo maarufu Billnass na nyota wa muziki wa Bongofleva Faustina Mfinanga maarufu Nandy wamefunga ndoa.
Wawili hao wamefunga pingu za maisha leo Julai 16, 2022 katika kanisa la KKKT Mbezi Beach, Dar es Salaam.
Nandy’ amejikuta akitokwa na machozi ya furaha madhabahuni wakati akila kiapo cha ndoa leo Julai 16, 2022 ambapo amefunga pingu za maisha na msanii William Lyimo maarufu kama Billnass.
Billnass na Nandy ni wapenzi wa muda mrefu na siku za hivi karibuni waliutangazia umma kuwa muda si mrefu watakuwa wazazi baada ya kupost picha zikimuonyesha Nandy akiwa mjamzito.
Picha: Clouds Digital
Social Plugin