Ndivyo
unavyo weza kusema wakati uchaguzi wa ndani ya CCM na jumuiya zake ukiendelea
kuanzia ngazi ya matawi, kata, wilaya hadi taifa. Kijana John Francis Haule (MIAKA
37), Ambaye ni kada wa ccm na mwkt wa
jumuiya ya wzazi wa tawi la nala chinagali Dodoma, amejitosa katika
kinyang’anyiro cha nafasi ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa.
Hayo yamejiri jana katika ofisi za wazazi taifa Jijini Dodoma wakati HAULE akirejesha fomu yake ya kugombea nafasi hiyo ndani ya jumuiya ya wazazi .
Akizungumza na mwandishi wa Ngasa online tv Ndg Haule alisema kuwa ameamua kuchukua fomu na kurejesha katika nafasi hiyo kwa kuwa anamaini kuwa ana uzoefu na nia ya dhati ya kuitumikia jumuiya hiyo na chama cha mapinduzi kwa ujumla wake.
Kwa mujibu wa Haule ambaye ni msomi wa shahada ya sayansi ya siasa na utawala (POLITICAL SCIENCE AND PUBLIC ADMINISTRATION DEGREE WITH HONOR. PSPA) ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Haule ambaye ni mzaliwa
wa Ludewa mkoani Njombe akiwa mwanachama hai wa CCM kuwa anatia nia kugombea
nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba ya ccm na jumuiya ya wazazi inayo toa haki kwa
kila mwanachama ya kuchagua na kuchaguliwa.
PONGEZI KWA RAIS NA
MWKT WA CCM TAIFA MH: SAMIA SULUHU HASAN
Ndg Haule wakati akizungumza kupitia Ngasa on line TV.allitumia fursa hiyo kutoa pongezi za thati kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake mzuri unaozingatia mifumo yote ya demokrasia,kwa mujibu wa Haule alibainisha kuwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kusema kuwa ili taifa lolote lipate maeendeleo linaitaji siasa safi na uongozi bora hivyo Mhe. Samia Suluhu Hassan ni mfuasi mahiri wa falsafa ya siasa safi nauongozi bora kama ilivyo wahi bainishwa na BABA WA TAIFA.
Pia Haule alisema kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kiigizo chema na
ni mfano mzuri wa kiongozi anayeongoza
Taifa kwa kuongozwa na sheria nasio kuiongoza sheria,na pia katika tawi la nala chinangali wana mwita kuwa ni ‘Malkia wa siasa safi wa karne hii ya 21’
MAONO JUU YA CCM NA
JUMUIYA YA WZAZI
Kwa mujibu wa HAULE maono yake juu ya CCM na jumuiya ya wazazi ya mejikita katika kitabu cha TUJISAHIHISHE 1962 Kilicho andikwa na Rais wa TANU J. K. NYERERE kikibainisha dhima ya ukweli kuwa hauna umri na unatabia ya kujilipiza kiasi ukipuuzwa.
Katika hilo Ndg Haule alisema kuwa CCM inapaswa kufanya maboresho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 hususni katika kipengele cha mgombea urais kuwa rais aliyoko madarakani anaye tokana na CCM ataendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitano ndani ya CCM bila kushindana na mwanachama mwingine yeyote ndani ya CCM.
Ili kuweza kuepuka dhana kwamba CCM ina tamaduni mana mwaka
2020 Ndg BERNAARD MEMBE alichalenge CCM
Kuwa CCM haiongozwi na tamaduni bali inaongozwa na katiba, so that was a challenge
aliongeza Haule na kusisitiza kuwa sasa niwakati muafafaka
wa KUJISAHIHISHA kwa jambo hilo.
Pia Haule alitoa ushauri kuwa pia kuwepo na ukomo wa Umri wa viongozi waandamizi ndani ya jumuiya na chama kwa ujumla wake.
“Endapo nitapata fursa ya kuwa Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa
nitashauri suala la ukomo wa umri kwa
viongozi waandamizi wa jumuiya na chama liwekwe kwenye katiba ya jumuiya ya
wazazi na CCM kwa ujumla wake”.
UZOEFU NA UTUKMISHI NDANI YA CCM NA JUMUIYA
ZAKE.
Kwa mujibu
wa HAULE kuwa asha hudumu katika nafai mbalimbali ndani ya accm kwa ujumla
1. 2022 Mwenyekiti wa umoja wa wazazi Tawi la nala
chinngali
2. Mjumbe wa
mkutano mkuu UVCCM wilaya ya Ilala Dar es salaam
3.Mjumbe
kamati ya fedha kata ya Ubungo Dar es salaam
4. Mjumbe
kamati ya utekelezaji umoja wa wzazi
tawi la Abiyani chuo kikuu
5.katibu UVCCM/CCM tawi la chuo kikuu
(Abuyani UDSM shirikisho la vyuo
vikuu)
6.Mjumbe wa
halimashauri kuu tawi la Mbuyuni Tabata Ilala
7.Mratibu na
katibu wa makongamano ya shirikisho vyuo vikuu Dar es salaa
"Kwa uzoefu
huu naamini unatosha kuiongoza jumuiya ya wazazi Tanzania", aliongeza Haule.
USIMAMIZI WA MIRADI YA
JUMUIYA YA WAZAZI
Jumuiya ya wazazi dhima yake kuu ni kupambana dhidi ya ujinga hivyo moja kati ya miradi ya jumuiya ni mashule yanayojulikana kama shule za wazazi , ambayo kwa kiasi kikubwa yamesaidia sana katika kuondoa adui ujinga.
"Hata mimi mwenyewe ni zao
la shule ya wazazi ambayo ni Ludewa Sekondari iliyoko mkoani Njombe wilayani Ludewa. Kwa kutambua
umuhimu huo nikiwa mwenyekit nitatoa msukumo wa
kasi ili kuziboresha Zaidi kimiundo mbinu, mfumo wa utawala pamoja na
namana ya ueendeshaji ili ziweze kueendelea kuwa kinara katikaka tasinia ya
elimu TANZANIA.
>Pia
kuanzisha miradi mingine ya jumuiya
kama vile ujenzi wa vituo vya afya vijijini(VILLAGE
MEDICS) Vyuo vya ufundi shabaha nikueendelea kuipiga jeki
serikali katika azma yake ya kuendeleaa
kuboresha maeendeleo ya nchi yetu na watanzania kwa ujumla.