KATIBU MKUU (OWM) PROFESA JAMAL KATUNDU ATEMBELEA PSSSF NA NSSF KWENYE MAONESHO YA SABASABA YANAYOENDELEA JIJINI

NA KHALFAN SAID, SABASABA

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu ametembelea banda la USHIRIKIANO linalotumiwa kwa pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam ili kujionea jinsi watumishi wa Mifuko hiyo iliyo chini ya Ofisi yake wanavyotoa huduma kwa wanachama wao na wananchi kwa ujumla.

Alipowasili kwenye banda hilo alipokelewa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF Bw. James Mlowe na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF Bi. Aisha Sango.

Profesa Katundu alitembezwa katika idara mbalimbali za mifuko hiyo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watoa huduma (watumishi), wananchama na wananchi waliotembelea banda hilo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja hivyo vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba.

Akiwa katika banda la PSSSF Profesa Katundu pia alijionea Tangawizi iliyochakwa inayozalishwa na kiwanda  kinachomilikiwa kwa ubiya baina ya PSSSF na wanaushirika wa Mamba Miamba, jimbo la Same mkoani Kilimanjaro ambapo alifurahia ubora wake.

Maonesho hayo ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yenye kauli mbiu isemayo “Tanzania Mahali Sahihi Pa Biashara na Uwekezaji,” yalianza Juni 28 na yanatarajiwa kufikia kilele Julai 13.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu, akifurahia jambo na mwanachama wa PSSSF aliyefika kuhudumiwa.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu (kushoto), akimsikilzia kwa makini Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Bw. James Mlowe alipotembelea banda hilo la Ushirikiano
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu (kulia), akimsikilzia kwa makini Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Bw. James Mlowe alipotembelea banda hilo la Ushirikiano. Kushoto ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Bi. Aisha Sango.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu (aliyeketi kushoto) akipatiwa huduma kwenye idara ya TEHAMA ya NSSF wakati alipotembeela banda hilo la USHIRIKIANO.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu (Kulia) akizungumza na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, PSSSF, Bw. James Mlowe
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu akiongozana na Bw. Mlowe, wakati alipotembelea band la USHIRIKIANO upande wa PSSSF na kuzunguzma na Wananchama na watumishi.

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Profesa Jamal Katundu, akihudumiwa na Afisa Mkuu wa Mafao NSSF Bi. Juleth Chalamila 

Mstaafu na mwanachama wa PSSSF akijaribu kutumia PSSSF kiganjani kupata huduma ndani ya panda la Mfuko huo.

Katibu Mkuu Profesa Jamal Katundu akiongozwa na Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma PSSSF, Bw. James Mlowe (kushoto) akipata maelezo kuhusu Tangawizi iliyochakatwa na kiwanda cha Tangawizi Mamba Miamba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post