Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza wakati akifunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) Prof. Penina Muhando akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Prof. Raphael Chibunda akizungumza katika Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wakuu wa Taasisi za Elimu nchini wakifuatilia hafla ya kufunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI inaendelea na programu mbalimbali za maboresho ya elimu ya vyuo vikuu nchini, ambapo katika mwaka huu wa fedha zaidi ya mitaala 300 inafanyiwa mapitio na kuhuishwa kwa kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali ili kukidhi matarajio yao na mahitaji ya soko.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael wakati akifunga Maonesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania yaliyokuwa yakiendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Amesema Wizara kupitia TCU itaendelea kutoa mafunzo ya kubadilishana uzoefu kwa wana taaluma wa vyuo vikuu kuhusiana na mbinu bora za ukusanyaji wa maoni ya wadau na vigezo vya uandaaji na uhuishaji wa mitaala itakayozingatia mahitaji ya wadau na soko la ajira.
“Wizara imesaini dola za kimarekani milioni 625 kwa ajili ya kujenga Vyuo Vikuu Vishiriki katika Mikoa ambayo isiyokuwa na vyuo vikuu, na Tanzania Bara na Zanzibar kote watapata vyuo vikuu vishiriki ambavyo baadae vitatanuka na kuwa vyuo vikuu,” Amesema
Aidha amesema Serikali imekuwa ikijivunia mafanikio makubwa katika sekta ya elimu kwa upande wa elimu ya juu imeimarisha mifumo ya udhibiti ubora wa elimu inayotolewa na elimu ya vyuo vikuu nchini ili kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Pamoja na hayo amesema Serikali kwa kushirikiana na TCU inawajibu wa kuendeleza maonesho hayo kila mwaka hivyo taasisi za vyuo vikuu viongeze muunganiko na vyuo vya nje ili kuwekeza kwenye elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) Prof. Penina Muhando amesema maonesho hayo yana lengo ya kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya taasisi zetu za elimu ya juu .
"Maonesho haya yatawezesha wananchi kupata fursa za kuona shughuli mbalimbali zinazotendwa na taasisi za elimu ili kuwasaidia wanaotaka kuendelea na elimu ya juu kufanya maamuzi ya kujiendeleza". Amesema Prof.Muhando.
Naye, Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA), Profesa Raphael Chibunda akizungumza kwa niaba ya washiriki wote alihimiza uwepo wa maonesho hayo kila mwaka kwa sababu yamekuwa yakisaidia bidadi ya wadahili kuongezeka.