Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAULI YA KWANZA YA HAJI MANARA BAADA YA KUFUNGIWA


Haji Manara

Msemaji wa Klabu ya Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara, amefungiwa kujihusisha na Mpira wa Miguu (Soka), Kwa kipindi Cha Miaka miwili na faini ya Shilingi Milioni 20.

Maamuzi ya kufungiwa kwa Manara yametangazwa leo Alhamis (Julai 21), na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ katika mkutano na Waandishi wa Habari.

Kamati ya Maadili ya TFF imebaini Haji alitumia Lugha ya vitisho dhidi ya Rais wa Shirikisho Wallace Karia wakati wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ kati ya Young Africans dhidi ya Coastal Union uliopigwa Julai 02 jijini Arusha, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

“Wewe unanifuatilia sana na hii ni mara ya tatu, hunifanyi lolote, huna uwezo wa kunifanya lolote.” Kauli ya Manara ambayo inadaiwa aliitoa dhidi ya Rais Karia

Baada ya adhabu hiyo,Haji Manara ametoa kauli ya kwanza baada ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutojihusisha na soka kwa miaka miwili ameandika haya;

“Iwe ni jambo la kheri au shari, neno langu kuu ni kumshukuru muumba mbingu na ardhi kwa neno moja kubwa na lenye maana pana sana. AL-HAMDULILLAH,”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com