Mike O'maera (EAPN) akifungua kongamano na utangulizi wa madhumuni ya kikao hicho. Wadau wakipiga picha kwenye hafla ya Tanzania Philanthropy Forum.
Karina Rupia ((TFC), Marcelina David (Kijana Jasiri Organisation) na Doris Mollel (Doris Mollel Foundation) wakijadili namna ya kutumia nguvu za jamii katika rasilimali za ndani na utandawazi.
Prudence Glorious, Afisa Mkuu wa Madhumuni wa PZG Impact Communications Firm, akiwasilisha mada kuhusu 'Nguvu ya Uhisani' na 'Mawasiliano ya Kimkakati.'
****************
Foundation of Civil Society (FCS), pamoja na East Africa Philanthropy Network (EAPN), waliandaa kongamano la pili la uhisani kwa mwaka huu - mnamo tarehe 21 Julai 2022. Tukio hilo lilikutanisha asasi za kiraia, kwa malengo ya kutoa elimu, kuchochea na kutoa hamasa juu ya suala la kujitolea kwa wanajamii, na wanajamii kutoa misaada kwenye masuala yanayokumba jamii zetu. Na pia kutoa elimu na hamasa juu ya namna za kutumia nguvu za jamii katika rasilimali za ndani na utandawazi.
Kati ya watu waliohudhuria kongamano ni Evans Okinyi, Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Philanthropy Network, ambaye aliomba wahudhuriaji kufanya mambo makuu matatu (3) "kuzalisha maarifa juu ya kutumia nguvu za jamii za ndani ya nchi kujitolea na kutoa msaada; kutia maanani ushirikiano na kuweka jamii mbele; pia kutumia majukwaa - kama EAPN - kuonyesha kazi zinazofanyika kusaidia jamii zetu."
Mojawapo wa wazungumzaji katika kongamano hilo alikuwa Prudence Glorious, Afisa Mkuu wa
Madhumuni wa Kampuni ya PZG Impact Communications Firm. Alisisitiza juu ya nguvu ya mawasiliano ya kimkakati katika kufikisha madhumuni yako ya kusaidia jamii kwa wadau - kupitia vyombo vya habari vya kuchapisha, vya sauti na mitandao ya kijamii.
Alielezea, "Unapowasilisha madhumuni yako ya kusadia jamii unahitaji kuwa na simulizi lenye kugusa hisia. Ni rahisi watu kuguswa kihisia na simulizi kwani ndivyo tunavyojenga uaminifu na mahusiano." Prudence alisisitiza, "Fahamu changamoto unazoshughulikia na tofauti ambayo shirika lako linaleta - kwa idadi na data. Unaweza kuzitoa idadi hizo wakati unapowasiliana na wadau wanaoweza kukusaidia na rasilimali kwa ajili ya shughuli zako za kutoa misaada."
Zaidi ya waleta mabadiliko 50 wa mashirika ya kiraia walihudhuria kongamano hilo. Miongoni mwao alikuwa Bi. Rose Nzali kutoka IOGT-NTO Movement EA. Bi Rose akiguswa na mawasilisho ya nguvu ya utoaji, na shuhuda juu ya athari iliyonayo, alichukua hatua ya kuchangia kwa Doris Mollel Foundation, huku akiwahimiza washiriki wengine waliohudhuria kuchangia pia.
Mwishoni mwa Kongamano hilo, Karin Rupia kutoka FCS, alishauri waliohudhuria kongamano hilo kujitokeza na kushughulikia masuala yanayohitaji msaada katika jamii zetu kwa kutumia zana ambazo tayari watu wanamiliki.
Pia aliwasihi wahudhuria kujumuisha wanafamilia na marafiki zao katika harakati za kutoa misaada.
Alisema hivi kuwasilisha kwamba uhisani, kujitolea na/au uchangiaji sio tu kuhusu kutoa rasilimali za kifedha bali ni kutoa nguvu na uwezo wako pia - kwasababu aina yoyote ya juhudi ndogo zinazowekwa katika kutoa msaada huleta mabadiliko makubwa.