Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akitembelea mabanda ya Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akisaini kitabu cha wageni kwenye moja ya mabanda ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi mara baada ya kutembelea mabanda ya Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
SERIKALI imejipanga kutekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa bandari ya Uvuvi ambayo itajengwa kwenye maeneo ya Kilwa Masoko mkoani Lindi ambapo mpaka kukamilika utachukua miaka miwili na utakuwa umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 266 ambazo zitatengwa na serikali katika kutekeleza mradi huo.
Ameyasema hayo leo Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah wakati alipotembelea mabanda ya Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Amesema bandari ya uvuvi ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya sekta ya uvuvi kwasababu inaendana na ule mkakati wa kufufua shirika la TAFICO ambapo wamepanga kununua meli ambazo zitaendeshwa na TAFICO kwa ubia na sekta binafsi.
Kuwekwa kwa bandari ya uvuvi kunavutia meli nyigi za nje na za ndani za watu binafsi ambazo zinakuja kuwekeza, kwasababu kwenye bandari ya uvuvi unapata mahali pekee ambapo meli inaweza kupata huduma zote za uvuvi .
"Bandari tulizonazo sasa hvi hamna bandari ya uvuvi , kwahiyo meli ikija ikitaka kushusha samaki ile miundombinu kama vyumba vya baridi au mitambo ya barafu haipo, sehemu ya kunywa mafuta haipo kwahiyo ile bandari italeta meli nyingi zitaweza kuwekeza". Amesema